Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Muziki wa Injili
Tanzania (CHAMUITA) kimeeleza kwamba Kamati ya maandalizi ya Tamasha la
Pasaka iliyo chini ya Kampuni ya Msama Promotions inatekeleza Neno
la Mungu na si Huduma kama inavyodhaniwa na Jamii.
Kwa Mujibu wa Mwenyekiti wa
Chamuita, Addo November ndio Maana Mwaka huu Wamelihamishia Tamasha hilo Mikoa ya Kanda ya Ziwa na kuachana na Dar es Salaam kama ilivyozoeleka.
November alisema kwa kuwa Msama
ameonesha kwamba Tamasha hilo ni sehemu ya Huduma Ametumia fursa hiyo
kuwaomba wakazi wa mikoa ya Geita, Mwanza na Wilaya ya Kahama na Mikoa
ya Jirani kujitokeza kwa wingi ili kupata Ujumbe wa neno la Mungu kutoka
kwa waimbaji Mbalimbali.
November alisema kampuni ya Msama
imejipambanua kwamba kupitia Tamasha la Mwaka huu kuwasaidia walemavu
ambako watakabidhiwa baiskeli zaidi ya 100.
Aidha naye Mwenyekiti wa Kamati
ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama alisema Wanaendelea na
mchakato wa kufanikisha ibada hiyo Muhimu kupitia Waimbaji na Viongozi
wa Dini.
Msama alisema Tamasha hilo
linatarajia kuanza Machi 26 mkoani Geita, Machi 27 Mwanza na Kahama
itakuwa Machi 28 ambako Waimbaji mbalimbali Wamethibitisha kushiriki
katika Tamasha hilo.
“Nawaomba wakazi wa Mikoa ya
Kanda ya ziwa kujitokeza kwa Wingi ili kufanikisha Msaada kwa Wenye Uhitaji maalum kama yatima, Walemavu na Wajane, hivyo wakazi wa mikoa Wajitokeze,” alisema Msama.
Msama alisema Viingilio katika Tamasha hilo ni shilingi 5000 kwa Wakubwa na Shilingi 2000 kwa Watoto
ambako Waimbaji Waliothibitisha kushiriki katika Tamasha hilo ni Rose
Muhando, Upendo Nkone, Bonny Mwaitege, Jesca BM, Joshua Mlelwa, Jenipher
Mgendi, Faustin Munishi, Kwaya ya Wakorintho Wapili na Kwaya ya AIC
Makongoro.
ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO
Robo Fainali ya Michuano ya Kombe
la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) inatarajiwa kuchezwa
wikiendi ya Mwisho wa mwezi Machi Mwaka huu, Huku Timu nane zikichuana
kusaka Nafasi ya kuingia Hatua ya Nusu fainali ya Michuano hiyo.
Machi 26, 2016 Utachezwa Mchezo Mmoja ambapo Wachimba dhahabu wa Geita Gold watakua Wenyeji wa Wachimba
Almasi wa mkoa wa Shinyanga timu ya Mwadui FC katika Uwanja wa CCM
Kirumba.
Alhamisi ya Machi 31, 2016, Young
Africans Watawakaribisha Ndanda FC katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es
salaam, huku timu ya Azam FC wakiwa Wenyeji wa Maafande wa Jeshi la Magereza Tanzania Prisons katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Mchezo wa Mwisho wa robo fainali
utachezwa Aprili 6, 2016 kwa Simba SC kucheza dhidi ya Coastal Union
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Aprili 7, 2016 itachezeshwa droo ya Hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) Mojamoja (live) katika Luninga.
Bingwa wa Michuano ya Kombe la
Shirikisho Msimu huu, ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la
Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) 2017.
Serikali yamkabidhi Cheka Cheti cha pongezi kutokana na ushindi wake.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(kulia) akiwa Ameambatana na
Bondia Francis Cheka (wapili kulia) alipotembelea Wizarani leo jijini
Dar es Salaam na Serikali imemkabidhi Cheti cha pongezi. Kushoto ni
Rais wa Chama cha ngumi Tanzania (TPBO) Yassin Adballah (Ustadh).
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(katikati) Akizungumza na
waandishi wa Habari Wakati wa Zoezi la kumkabidhi Cheti cha pongezi
kutokana Na ushindi Bondia Francis Cheka (kushoto) leo jijini Dar es
Salaam.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex
Nkenyenge.
Bondia Francis Cheka akizungumza
na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) Wakati wa zoezi la kupokea
Cheti cha pongezi kutoka kwa Serikali leo jijini Dar es Salaam. Kutoka
kulia ni Waziri Wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye,Rais wa Chama cha ngumi Tanzania (TPBO) Yassin Adballah (Ustadh)
na Meneja wa Bondia huyo Chifu Ndambile Juma Ntinginya.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wapili kushoto) Akimsikiliza
kwa makini Katibu Mtendaji wa BMT Mohamed Kiganja (aliyesimama)
akizungumza Na waandishi wa Habari wakati wa zoezi la kumkabidhi Cheti
cha pongezi Bondia Francis Cheka (kushoto) kutokana na ushindi wa Mkanda
wa Uzito wa Super Middle wa Mabara wa WBF leo Jijini Dar es Salaam.
Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akimkabidhi Cheti cha
pongezi Bondia Francis Cheka kutokana na ushindi alioupata katika
pambano baina yake na Bondia Mserbia anayeishi Uingereza Geard Ajetovic
(hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) na Bondi Francis Cheka
wakiwaonyesha waandishi wa Habari Mkanda wa uzito wa Super Middle wa
Mabara ambao Cheka ameunyakuwa baada ya kushinda pambano la tarehe 27
Februari baina Yake na Bondia Mserbia anayeishi Uingereza Geard Ajetovic
(hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa Bondia
huyo Chifu Ndambile Juma Ntinginya.
No comments:
Post a Comment