Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Uganda
Yoweri Museven baada ya kuwasili katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani
Arusha Palipofanyika mkutano wa 17 wa Nchi za Afrika ya Mashariki
EAC,(kulia) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe
Magufuli,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein baada ya kuwasili
katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha palipofanyika mkutano wa 17 wa
Nchi za Afrika ya Mashariki EAC,[Picha na Ikulu.]
Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika
ya Mashariki wakisimama wakati wimbo wa umoja wa nchi hizo ukipigwa
katika mkutano wa 17 wa EAC uliofanyika leo ukumbi wa Ngurdoto mkoani
Arusha,[Picha na Ikulu.]
Miongoni mwa Mawaziri wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
walioalikwa katika mkutano wa 17 wa Viongozi wakuu wa nchi za Afrika ya
Mashariki EAC uliofanyika leo ukumbi wa Ngurdoto Hotel Mkoani
Arusha,(katikati) Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora
Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini,akiwa na Mawaaziri wa Nchi za Jumuiya
hiyo,{Picha na Ikulu.]
Rais Magufuli akutana na kufanya Mazungumzo na Rais Kenyatta na Rais Kagam
Viongozi Wakuu wa Nchi za Afrika
ya Mashariki akiwemo mwenyekiti wa mkutano wa 17 wa EAC Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kabla ya kuanza kwa Mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Ngrdoto Mkoani
Arusha,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri
ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, kando ya Mkutano Mkuu wa 17 wa
kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
unaofanyika Mkoani Arusha, ambapo viongozi hao wamekubaliana kuimarisha
mahusiano hususani katika masuala ya kiuchumi.
Baadhi ya maeneo waliyokubaliana
kutilia mkazo katika mahusiano hayo, ni pamoja na kutekeleza miradi ya
maendeleo inayounganisha nchi mbili ikiwemo ujenzi wa miundombinu,
kukuza biashara na kuzalisha ajira kupitia viwanda.
Rais Uhuru Kenyatta amesema
amefurahishwa sana kuona Rais Magufuli yupo tayari kuhakikisha nchi ya
Kenya na Tanzania zinakuwa karibu, na miradi ya maendeleo inaharakishwa.
“Kwa sababu nia yetu sisi ni
kuona maendeleo ambayo yatagusa mwananchi wa kawaida, tumalize
umasikini, uchumi ukue, na hivyo hatuwezi kufanya tukiwa tumetengana” Amesisitiza Rais Kenyatta.
Kwa upande wake Rais John Pombe
Magufuli, amesema Tanzania na Kenya zina kila sababu ya kuimarisha
mahusiano ya kibiashara hasa katika ujenzi wa viwanda utakaozalisha
ajira kwa kuwa watu wake ni wamoja.
“Wazee wetu Mzee Kenyatta na
Mzee Nyerere walijenga mazingira mazuri ya kuwa na nchi hizi Mbili
wakati wakipigania uhuru, sasa sisi vijana wao ni wakati wetu kwenda
mbele kwa ajili ya maendeleo” amebainisha Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli amebainisha kuwa
nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinajenga Mahusiano na
ushirikiano zinalenga kupata manufaa hayo ya kiuchumi kwa manufaa ya
wananchi wake.
Ameutaja mradi mmojawapo kuwa ni
ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Tanzania kwenda nchini Kenya
kupitia Namanga, na akaongeza kuwa Tanzania itakapoongeza uzalishaji wa Umeme na kuanza kuvuna gesi, itaiuzia pia Kenya, halikadhalika Kenya
nayo itauza bidhaa zake Tanzania.
Kabla ya kukutana na Rais
Kenyatta, Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Wa
Jamhuri ya Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame, ambapo viongozi hao
wamekubaliana kuzidisha mahusiano kati ya Tanzania na Rwanda ambapo Rais
Magufuli amemhakikishia kuwa Serikali yake itakamilisha ujenzi wa Reli
ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani “Standard Gauge” ili kurahisha
usafirishaji wa bidhaa na watu.
Rais Kagame amempongeza Rais
Magufuli kwa uongozi wake bora uliolenga kuimarisha uchumi, ikiwemo
kuimarisha bandari ya Dar es salaam ambayo Rwanda inaitegemea na ujenzi
wa Reli ya Kati ambayo pia ni tegemeo kubwa kwa uchumi wa Rwanda.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiano, IKULU
Arusha
02 Machi, 2016
No comments:
Post a Comment