Saturday, 27 February 2016

Gavana wa New Jersy amuunga mkono Trump

   

Katika kile kinachoonekna kama hatua ya kushangaza katika kinyanganyiro cha urais nchini Marekani Gavana wa jimbo la New Jersey Chris Christie amemuunga mkono billionea Donald Trump katika uteuzi wa Chama cha Republican.

Bwana Trump aliitaja hatua hiyo kama aliyokuwa akiihitaji zaidi.
Wawili hao walikuwa mahasimu hadi wiki mbili zilizopita wakati bwana Christie alifutilia mbali kampeni yake.
Bwana Christie alisema kuwa Trump alikuwa katika nafasi bora ya kumshinda Hillary Clinton ambaye Anatafuta nasafi ya kuwania urais kupitia chama cha Democratic.

Hio leo Clinton Atatafuta Uteuzi katika Jimbo la South Carolina ambalo Bwana Trump alishinda kupitia Chama cha Republican.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ziara ya siku moja Mtwara

MTW1
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Mtwara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege ea Mtwara kwa ziara ya siku moja mkoani humoFebruari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Rais Mpya Wa FIFA ni Gianni Ifantiano

fi1
Gianni Infantino ndiye aliyechaguliwa kuwa rais mpya wa shirikisho la soka duniani Fifa
Raia wa Switzerland Gianni Infantino amechukua mahala pake Sepp Blatter kama rais wa shirikisho la soka duniani Fifa.katibu huyo mkuu wa Fifa alipata kura 115 katika raundi ya pili ikiwa ni kura 27 zaidi ya mpinzani wake wa karibu Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa.
Mwanamfalme Ali bin al-Hussein alikuwa wa tatu akiwa na kura nne huku Jerome Champagne akishindwa kupata hata kura moja. Tokyo Sexwale alijiondoa kabla ya kura kuanza kupigwa mjini Zurich.
fi2
Infantino akiwashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa FIFA
Raundi ya kwanza ya upigaji kura ilishindwa kum’baini mshindi wa moja kwa mojaWingi wowote wa kura[zaidi ya aslimia 50] katika raundi ya pili ya uchaguzi huo ulikuwa unaweza kumwezesha mgombea kutangazwa mshindi katika raundi ya pili.
Infantino ni wakili mwenye umri wa miaka 45 kutoka eneo la Brig jimbo la Valais nchini Switzerland ,ikiwa ni eneo lililopo chini ya maili sita kutoka nyumbani kwa Blatter.
Blatter ambaye aliliongoza shirikisho hilo tangu mwaka 1998 alijiondoa mwaka uliopita kabla ya kupigwa marufuku katika shughuli zozote za kandanda kwa kipindi cha miaka sita .
FI3
Infantino akiwahutubia wajumbe
Baada ya kutangazwa mshindi, Infantino aliwaambia wajumbe waliopiga kura kwamba hakuweza kujielezea kutokana na hisia alizokuwa nazo.
Lakini aliwaambia wajumbe kwamba ”kwa pamoja wataweza kuirudisha sura ya Fifa na heshima ya Fifa’

MWANAMUZIKI WA ZAMANI KASSIM MAPILI AZIKWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

map1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiweka udogo kwenye kaburi la Mwanamuziki mkongwe hapa nchini, Mzee Kassim Said Mapili, wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam leo.
map2
Mwili wa mwanamuziki mkongwe hapa nchini, Mzee Kassim Said Mapili ukiwasili kwenye makabuli ya Kisutu, jijini Dar es Salaam leo.
map3
Mwili wa mwanamziki mkongwe hapa nchini, Kassim Said Mapili ukiwekwa katika kabuli wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye makabuli ya Kisutu, jijini Dar es Salaam leo.
map4
Waombolezaji waliofika kumsindikiza kwenye nyumba ya milele  Mzee Kassim Said Mapili, wakipata mawaidha baada ya mazishi.
  Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimfariji mtoto wa marehemu
  Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimfariji mtoto wa marehemu
  Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipeana mikono na mwanamuziki mkongwe Mjusi Semboja huku akiongea na Mzee Makassy na wanamuziki wengine
 Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiongea na mchambuzi wa muziki wa dansi mahiri Zomboko na mdau wa muziki Hassan.

MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI

d02
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa dini kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salam Februari 26, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
d01 d1
 Baadhi ya viongozi wa dini wanaunda kamati ya amani ya Dar es salam na baadhi ya mikoa nchini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
d2
 Baadhi ya viongozi wa dini wanaunda kamati ya amani ya Dar es salam na baadhi ya mikoa nchini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
d3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu, Elinaza Sendoro baada ya kuzungumza na Viongozi wa Dini kwenye Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
d4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu, Alex Molasses baada ya kuzungumza na Viongozi wa Dini kwenye Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
d5
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini baada ya kuzungumza nao kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyererejijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
d6
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini baada ya kuzungumza nao kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyererejijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
d7
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini baada ya kuzungumza nao kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyererejijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAWAZIRI WOTE WAJAZA TAMKO LA MALI NA MADENI

c38d70b6-1ea3-40f3-a8b2-95c9813523f8
Na Kalonga Kasati
 Waziri MKUU Kassim Majaliwa amesema agizo lilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli la kuwataka mawaziri ambao hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni wakamilishe kabla ya saa 12 leo jioni limetekelezwa.

Waziri Mkuu amepokea barua kutoka kwa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji (Mst.) Salome Kaganda ikithibitisha kuwa mawaziri na naibu mawaziri wote wametekeleza agizo hilo.

“Hadi kufikia saa 9.30 leo alasiri (Ijumaa, Februari 26, 2016) mawaziri wote walikuwa wamekamilisha fomu zao za kuzikabidhi katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,” alisema Waziri Mkuu.

Rais Magufuli leo asubuhi alitoa maelekezo kwamba Mawaziri ambao hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni ifikapo leo Ijumaa tarehe 26 Februari, 2016 saa 12.00 jioni wawe wamejaza na kurejesha Fomu ya Tamko la Rasilimali na Madeni katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Dar es Salaam. Waziri ambaye atashindwa kutekeleza agizo hili atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi yake.

Friday, 26 February 2016

Wagombea watano wanawania kumrithi Sepp Blatte leo

 Fifa

Shirikisho la soka duniani Fifa litampta kiongozi mpya leo wajumbe 207 watakapokusanyika mjini Zurich, Uswizi kumchagua mrithi wa Sepp Blatter.

Blatter, 79, aliongoza shirikisho hilo tangu 1998.

Aling’atuka mwaka Jana kutokana na Tuhuma za ufisadi zilizogubika shirikisho hilo.
Kuna wagombea watano wanaotaka kumrithi.
Watano hao ni Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa, Gianni Infantino, Mwana mfalme Ali bin al-Hussein, Tokyo Sexwale na Jerome Champagne.

Sheikh Salman na Gianni Infantino ndio wanaopigiwa upatu kushinda.
Upigaji kura utaanza saa 12:00 GMT (saa tisa alasiri saa za Afrika Mashariki).
Kabla ya kura kupigwa, kila mgombea atakuwa na dakika 15 za kuhutubia wajumbe.

Kuna Mataifa 209 wanachama wa FIFA lakini Kuwait na Indonesia kwa sasa hawashirikishwi, hivyo wajumbe watakaopiga kura ni 207.

Ili kutangazwa mshindi duru ya kwanza, mgombea anahitaji kupata theluthi mbili ya kura zilizopigwa.
Hili lisipofanyika, wagombea wote wanapigiwa kura tena duru ya pili na anayepata kura nyingi kutangazwa Mshindi.

Mshindi akikosekana duru ya pili, basi duru ya tatu hufanyika bila mgombea mwenye kura chache zaidi Raundi ya pili.

Fifa imesema lazima mshindi ajulikane leo Ijumaa.

Basata Wamlilia Mapili

mapi
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha Msanii Mkongwe wa muziki wa dansi Kassim Mapili kilichotokea katikati ya wiki hii nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam.

Na Tabu Mullah
 
Kassim Mapili ni msanii na mdau wa muda mrefu wa sekta ya Sanaa nchini. Amekuwa ni taa na nuru ambayo katika kipindi chote cha uhai wake imeangaza na kutoa mwanga angavu kwenye sekta ya Sanaa.

Mchango wake katika muziki wa dansi na ule wa kiweledi katika kuandaa na kukuza bendi na wasanii mbalimbali wa muziki wa dansi nchini hautasahaulika kamwe. Ni Msanii aliyeacha alama kuu katika muziki wa bendi na amejitolea kwa kiasi kikubwa katika kuufikisha muziki wa dansi ulipo leo.

Aidha, pamoja na kuwa mwimbaji na mpigaji gitaa katika Bendi mbalimbali zikiwemo za Kilwa Jazz, Polisi Jazz, Vijana Jazz na nyingine nyingi Mzee Kassim Mapili alikuwa mstari wa mbele kujenga mfumo wa Utawala kwenye sekta ya Sanaa na kuhakikisha wasanii wa muziki wa dansi wanakuwa na chombo cha kuwawakilisha na kutetea maslahi yao.

Mwaka 1982 alikuwa miongoni mwa wasanii waliokutana Mjini Bagamoyo na kuunda Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA) ambacho hadi leo kinatetea na kuwawakilisha wasanii wa muziki wa dansi.

Aidha, Mzee Mapili amekuwa bega kwa bega na Baraza la Sanaa la Taifa katika programu zake mbalimbali na utendaji kazi wa kila siku. Kwa mfano; amekuwa mmoja wa wadau ambao wamekuwa wakishiriki kikamilifu kwenye Programu ya Jukwaa la Sanaa inayoandaliwa na BASATA kwa kushirikiana na chama cha waandishi wa habari za Sanaa na Utamaduni.

Baraza, wasanii na wadau wote wa Sanaa hatuna budi kuendelea kuenzi mema yote aliyotuachia marehemu Kassim Mapili hasa katika kutunga nyimbo za hamasa na ujumbe makini na wenye mashiko kwa jamii yote ya Watanzania
.
Hakika pengo lililoachwa na Marehemu haliwezi kuzibika, kwani imekuwa ni kama mshumaa uliyozimika ghafla wakati tukiingia kwenye giza.

Baraza linatoa pole kwa familia ya Marehemu, chama cha muziki wa dansi, shirikisho la muziki na wasanii wote kwa ujumla. Ni matumaini ya Baraza kwamba, tutaendelea kuenzi mema yote yaliyotendwa na Marehemu, hasa kudumisha upendo na amani katika tasnia yetu ya Sanaa na taifa kwa ujumla.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Amen
Godfrey Mngereza
KATIBU MTENDAJI

Rais Dkt John Pombe Magufuli amlilia mzee Kassim Mapili

mapi

KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI CHAFANYIKA LEO.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Jesh Lupembe akizungumza katika kikao cha baraza la Madiwani wa Halamshauri hiyo.
Baadhi ya watendaji wa Halmashari ya Manispaa ya Moshi wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo .
Baadhi ya Madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakifuatilia kwa makini hoja zilizokuwa zikitolewa  katika kikao cha baraza hilo.
Diwani wa kata ya Ngangamfumuni ,Anthony …….akichangia hoja katika kikao cha bajeti cha Halmashauri ya manispaa ya Moshi .
Diwani wa kata ya Ng’ambo ,Genesis Kihwelu akichangia hoja katika kikao hicho.
Diwani wa kata ya Kilimanjaro,Priscus Tarimo akifuatlia hoja katika kikao hicho.
Msathiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya (Kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ,Jesh Lupembe.
Diwani wa kata ya Kiusa ,Stephen Ngasa akichangia hoja katika kikao hicho.
Diwani wa kata ya Mji Mpya ,Abuu Shayo akichangia hoja katika kikao hicho.
Baadhi ya Madiwani wakifuatilia michango ya madiwani wenzao katika kikao hicho.
Diwani wa kata ya Miembeni,Mbonea Mshana akichangia hoja katika kikao hicho.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya akiwa katika kikao hicho.
Diwani wa kata ya Bondeni Masiu Kilusu akifuatilia hoja za madiwani wenzake.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafry Michael pia laikuwa ni miongoni mwa madiwani waliohudhuria kikao hicho.
 

Waziri Kitwanga Akutana na Vionozi wa nida awataka kuongeza kasi Uandaji wa Vitambulisho vya Taifa

KTG1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Mamlaka hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wa kwanza upande wa kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira akifuatiwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modest Kipilimba. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KTG2
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Mamlaka hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira akifuatiwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wizarani hapo, Haji Janabi. Wa tatu kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modest Kipilimba, anayefuata ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Avelin Momburi na Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho, Paul Bwathondi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KTG3
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modest Kipilimba akijitambulisha kabla ya kuanza kikao cha Watendaji Wakuu wa NIDA pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kikao hicho kilichoitishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na anayefuata ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KTG4
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza jambo katika kikao kazi alichokitisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) kuzungumza na Watendaji Wakuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara yake, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya NIDA na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wa tano kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modest Kipilimba. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MAKAMBA AKUTANA NA BALOZI WA KUWAIT NCHINI

JAN1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. January Makamba (kushoto) akiongea na Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Al-Najem, Balozi huyo alimtembelea Mh. Makamba Ofisini kwake leo Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadiliana masuala ya hifadhi na usimamizi wa Mazingira.
JAN2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. January Makamba (kushoto) akiongea na Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Al-Najem, Balozi huyo alimtembelea Mh. Makamba Ofisini kwake leo Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadiliana masuala ya hifadhi na usimamizi wa Mazingira. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makumu wa Rais Bw. Mbarak Abdulwakil na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Barthlomew Jungu.

Badilisheni Sera zenu Muandike Habari chanya kwa watu wenye Ulemavu: Dkt Possi

PO1
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt  Abdallah Possi akizungumza na Wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari leo ofisini kwake Jijini Dare s salaam.
PO2
Mhadhiri toka Chuo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Shule ya Uandishi wa Habari Dkt Harub Riyoba (katikati) akimsikiliza Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt  Abdallah Possi alipokutana na Wamiliki wa Vyombo vya habri kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji toka Azam Media Yahya Mohamed na kushoto ni Meneja wa Uendeshaji toka Sahara Media Steve Diallo.


Na Kalonga Kasati
 
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt  Abdallah Possi ameviagiza vyombo vya habari nchini kuwa na sera katika vyombo vyao inayojumuisha uandishi wa habari chanya kwa watu wenye ulemavu.
 
Akitoa agizo hilo mbele ya wamiliki wa vyombo vya habari leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam Waziri Possi amesema habari nyingi zinazohusu watu wenye ulemavu ni za kuwanyanyapaa na kuonesha kuwa hawana uwezo wa kufanya mambo chanya.
 
“Wekeni kipengele katika sera zenu kitakachosaidia kuwaelimisha watu kuwa watu wenye ulemavu ni sehemu ya jumuiya katika maisha ya kila siku ya wanadamu,” amesema.
Kwa mujibu wa Waziri Possi, vyombo vya habari vikiwa na sera iliyowazi na kuitekeleza, watu watabadilika na kupata taarifa nzuri za watu wenye ulemavu.
 
Dkt. Possi ameeleza kuwa taarifa za watu wenye ulemavu hazitakiwi kuwa na lugha zenye chembechembe za kunyanyapaa.
 
Amesema kuwa kila kituo cha televisheni kinatakiwa kuwa na wataalamu wa kutafsiri habari na vipindi muhimu kwa lugha za alama.
 
Amesema, “Serikali kwa kutumia Sheria ya Watu wenye ulemavu Na. 9 ya mwaka 2010 inaandaa tangazo kuvikumbusha vyombo vya habari kuwa kuwa na wataalam wa kutafsiri habari na vipindi muhimu kwa lugha za alama kwa watu wenye ulemavu.” 
 
Aidha Naibu Waziri amewaagiza wamiliki wa vyombo vya habari kutoa ajira kwa watu wenye ulemavu kwani Sheria inaagiza lazima chombo chochote chenye wafanyakazi zaidi ya 20, angalau mfanyakazi mmoja awe mtu mwenye ulemavu.
 
Kwa upande wao wamiliki wameiomba serikali kutotoza kodi tangazo lolote linalohusu habari chanya za watu wenye ulemavu.
 
Hata hivyo wamiliki hao wamemweleza Naibu Waziri kuwa ubadilishaji wa Sera pamoja na kuwa na wataalam wa kutafsiri habari na vipindi muhimu kwa watu wenye ulemavu ni jambo zuri, lakini wanahitaji kupewa muda wa maandalizi.

Waziri Nape aahidi upatikanaji wa Sera ya Filamu nchini.

fiso1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwasili eneo la tukio kushuhudia uchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) uliofanyika 25 Februari, 2016 Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Bi. Joyce Fissoo.
fiso3
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (mwenye suti nyeusi) akiwahutubia Wasanii pamoja na wageni waalikwa wakati wa siku ya uchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) uliofanyika 25 Februari, 2016 Jijini Dar es Salaam.
fiso4
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Bi. Joyce Fissoo (kushoto) akiwahutubia Wasanii pamoja na wageni waalikwa wakati wa siku ya uchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) uliofanyika 25 Februari, 2016 Jijini Dar es Salaam.
fiso5
Viongozi wa Uchaguzi wakitoa maelekezo juu ya namna zoezi la upigaji kura kwa kiti cha Rais, Makamu wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF).
fiso6
Viongozi wa Uchaguzi wakitoa maelekezo juu ya namna zoezi la upigaji kura kwa kiti cha Rais, Makamu wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF).
fiso7
Baadhi ya Wasanii toka vikundi mbalimbali katika baadhi ya mikoa wakifuatilia kwa makini zoezi la upigaji kura pamoja na sera na vipaumbele vya Wagombea wa ngazi mbalimbali wakati wa uchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) uliofanyika 25 Februari, 2016 Jijini Dar es Salaam.
fiso8
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba (kulia) akihitimisha ukomo wa Serikali yake ya Shirikisho hilo kabla ya upigaji kura kuanza siku hiyo ya 25 Februari, 2016.

Na Tabu Mullah
Katika kuhakikisha kuwa Sekta ya Filamu nchini inakua kwa kasi na kuleta manufaa kwa wasanii, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amewahakikishia wasanii juu ya kupatikana kwa Sera ya filamu ili kuleta matokeo chanya ya katika kazi zao.

Mhe. Nnauye ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) ambapo ameahidi kushirikiana na Shirikisho hilo katika nyanja mbalimbali na kuwataka wanachama kuchagua viongozi wawajibikaji watakaoweza kusimamia Katiba kwa maslahi ya wote.

“Chagueni viongozi wenye weledi, wawajibikaji na wachapakazi ili mshirikiane nao katika kuleta maendeleo  kutokana na kazi zenu kitaifa na kimataifa”, alisema Mhe. Nnauye.
Aidha, Mhe. Nnauye ameahidi kutatua tatizo la usambazaji wa kazi feki za filamu ulioenea kwa kasi  nchini  ambapo amesema kwa kushirikiana na wadau wa filamu nchini yaani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bodi ya Filamu pamoja na COSOTA  watahakikisha kuwa, kazi ambayo haina ubora haingii sokoni.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu, Bi. Joyce Fissoo  ameeleza kuwa, Serikali  itasimamia kwa umakini filamu za nchini kwa kutoa mafunzo kwa vijana na Shirikisho ili waelewe majukumu yao na jinsi ya kufanya kazi kwa weledi.

Bi. Fissoo ameongeza kuwa nidhamu katika kazi ni muhimu kwa wasanii kwa kuwa inaleta heshima kwao na kwa Taifa, hivyo ni wajibu wa kila msanii kufuata maadili ili kuzalisha kazi nzuri zitakazopata soko ndani na nje ya nchi.

“Kuwepo katika Vyama ni msingi mkubwa wa mafanikio, fuateni Katiba,  tafuteni vipaumbele katika kazi zenu na pia zingatieni muda kwa kila mtakalofanya, naamini  mtafanikiwa’’, alisema Bi. Fissoo.

Shirikisho la Filamu Tanzania lilifanya uchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais na wajumbe kumi wa Bodi Februari 25 mwaka huu,  ambapo Bw. Simon Mwakifwamba alitetea nafasi yake ya kiti cha Urais wa Shirikisho hilo kwa muhula wa miaka mine (2016-2020) na Bw. Deo Sanga kuwa makamu wa Rais.