Friday, 2 June 2017

Wabunge wa Upinzani Watoka Nje

Mbunge John Mnyika atolewa nje ya Bunge kwa amri ya Spika Job Ndugai na kuamriwa kutohudhuria vikao kwa siku 7 baada ya kutokea malumbano leo.
Kufuatilia tukio hilo Wabunge wa Upinzani wametoka nje baada ya Mbunge huyo kutolewa nje na Askari wa Bunge kwa amri ya Spika.
Vilevile, Mamlaka ya Bunge kupitia Kamati ya Maadili kumjadili Mbunge Esther Bulaya kwa kuhamasisha wabunge kutoka nje ukumbi wa Bunge

Kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa

unnamed
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro akitoa muhtasari wakati wa ufunguzi wa kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
unnamed
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
2
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
 
4
Ukumbi wote ukimsikiliza kwa makini wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
 
5
 Meza kuu ikimpongeza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
unnamed
Kamishna wa Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar Afande Hamdan Omar makame akitoa shukurani kwa niaba ya wote kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017.
 
0
Kamishna wa Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar Afande Hamdan Omar makame akipeana mikono na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kumshukuru kwa niaba ya wote kwa kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
1
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu akipata picha ya pamoja na Makamishna wa Jeshi la Polisi baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
 
2
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu akipata picha ya pamoja na Makamishna, makamanda wa Wakuu wa Vikosi wa Jeshi la Polisi baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu akipata picha ya pamoja na Makamanda wa Polisi wa mikoa baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu akipata picha ya pamoja na Makamanda wa Vikosi vya  Polisi baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
6
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaga baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 20 
 
PICHA ZOTE NA IKULU

Mazoezi ya Taifa Stars

unnamed
Mshambuliaji wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbaraka Yussuf Abeid (katikati) ‘anaposepa’ na kijiji yaani kuhama au kuondoka na idadi kubwa ya watu/mabeki waliomzunguka wakiwamo Salum Mbonde, Shomari Kapombe na Kiungo Aboubakar Salum katika mazoezi ya timu yanayofanyika Uwanja wa mazoezi wa Kituo cha michezo cha Tolip (Tolip Sports City) hapa Alexandria, Misri. Taifa Stars  inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti kutoka Kampuni ya Bia ya SBL inajiandaa kucheza na Lesotho Juni 10, 2017 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon. Picha na Alfred Lucas wa TFF.

Mpaka leo asubuhi Juni 2, mwaka huu, Kocha Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga pamoja na wenzake katika benchi la ufundi, wamekinoa kikosi hicho kwa dakika 420 ndani ya Uwanja wa mazoezi wa Kituo cha michezo cha Tolip yaani Tolip Sports City hapa Alexandria, Misri.
Kwa mujibu wa programu ya Kocha Mayanga, Taifa Stars  inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti kutoka Kampuni ya Bia ya SBL itafanya mazoezi yasiyopungua dakika 1,500 katika kambi iliyoanza Mei 31, 2017 usiku na kufikia kikomo Juni 7, mwaka.
Siku ya kwanza ya kambi Mei 31, mwaka huu Kocha Mayanga alianza na dakika 120 za mwanzo baada ya kusafiri salama kutoka Tanzania hadi hapa Misri.
Kila siku Taifa Stars ina programu mbili ambako asubuhi timu inafundishwa kwa dakika 90 uwanjani kwa mazoezi mbalimbali na kwa programu ya usiku ni dakika 120 ambako huanza saa 3.00 (saa 2100) usiku na kumaliza saa 5.00 (saa 2300) usiku kwa saa za hapa Misri.
Kwa msingi huo, Kocha Mayanga kwa kusaidiana na benchi lake la ufiundi, anakionoa kikosi hicho kwa takribani saa 25 kwa wiki, kabla ya kurejea nyumbani. Timu itarudi Tanzania usiku wa kuamkia Juni 8, mwaka huu.
Ikiwa nyumbani Tanzania, Mayanga atawanoa tena kwa dakika nyingine 180 tayari kabisa kuivaa Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo umepangwa kuanza saa 2.00 usiku.
Mchezo dhidi ya Lesotho ni muhimu kwa Tanzania ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi ‘L’ kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.
Mbali ya Lesotho na Tanzania, mataifa mengine katika Kundi ‘L’ ni Uganda na Cape Verde ambao pia wikiendi ya Juni 9, 10 na 11, mwaka huu watakuwa katika mchezo wa kwanza pia kuwania nafasi hiyo.
Akizungumza mwenendo wa mazoezi kwa saa 300 za mwanzo, Kocha Mayanga amesema: “Nafarajika vijana wangu wameendelea kufunguka. Hapa hawana usumbufu wo wote, ni mazoezi na kupumzika kulingana na ratiba na chakula.”
Mazoezi ya Mayanga hayathiri maendeleo ya mwili wa binadamu kadhalika nguzo ya funga kwa wale ambao wako kwenye mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kwani ratiba huonyesha huanza kunolewa kuanzia saa 12.00 alfajiri – saa mbili baadaye baada ya daku (Uhudumiwa daku kabla ya saa 11.00 alfajiri), lakini pia saa 3.00 usiku ikiwa ni saa mbili baada ya kufuturu (Futari ni saa 12.45 jioni).

Balozi wa Morocco akutana na Rais DK.Ali Mohamed Shein

unnamed
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akisalimiana na mgeni wake Balozi wa Morocco katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Abdelilah Benryane wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akizungumza na mgeni wake Balozi wa Morocco katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Abdelilah Benryane wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.]02/06/2017.

sheria ya Vyombo vya Moto kufanyiwa Marekebisho

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji
  Serikali imeahidi kuifanyia marekebisho sheria inayoagiza tozo ya umiliki wa vyombo vya moto (road license) ili kuondoa kero kwa wananchi.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema hayo bungeni leo (Ijumaa) alipojibu swali la Dk Raphael Chegeni aliyetoa pendekezo hilo ili kodi hiyo iendane na matumizi halisi ya vyombo vya moto barabarani.
"Tozo hii ipo kisheria. Serikali imesikia mapendekezo ya wabunge na itaangalia namna nzuri ya kuboresha ukusanyaji wa mapato hayo," amesema Dk Kijaji.

Ufilipino: Watu 36 wafariki katika chumba cha kuchezea kamari

Kituo cha kamari cha Resorts World Manila kimewekwa chini ya ulinzi mkali baada ya kisa hicho
Watu 36 wameuawa katika kituo cha kuchezea kamari mjini Manila, Ufilipino baada ya mtu mwenye silaha kuanza kuwafyatulia risasi watu waliokuwemo humo.
Wengi wa waliofariki inaaminika wamefariki kutokana na kukosa hewa safi kutokana na moshi uliotanda mwanamume huyo alipowasha moto meza za chumba hicho cha kamari.
Mwanamume huyo alianza kwa kupiga risasi skrini za TV katika chumba hicho cha Resorts World Manila mapema Ijumaa.
Polisi wanasema baadaye alijiteketeza.
Kisa hicho kimesababisha kuanzishwa kwa operesheni kali ya kiusalama.
Maafisa awali walisema hakuna aliyekwua ameumia kutokana na kisa hicho, lakini sasa inabainika kwamba wamepataa miili ya watu wakikagua chumba hicho.
Polisi wanasema kisa hicho kinaonekana kuwa kisa cha kawaida tu cha wizi, na kwamba hakikuhusiana na ugaidi.
Watu zaidi ya 50 wamepelekewa hospitalini wakiuguza majeraha.
Mwanamume huyo alionekana kwenye kamera za CCTV ndani ya chumba hicho
Shambulio lilitekelezwa vipi?
Maafisa wanasema mwanamume huyo, ambaye jina lake halijatajwa kufikia sasa, aliingia ukumbi wa kituo hicho na kuanza kufyatulia risasi skrini za runinga mwendo wa saa sita usiku. Watu waliokuwemo ndani walianza kukimbia.
Pia alichoma moto meza za kamari na kujaza mkoba wake na vipande vya kuchezea kamari vya thamani ya peso milioni 113 za Ufilipino (£1.7m, $2.3m).
Baadaye alikimbia na kuingia upande wa kituo hicho wenye hoteli, akaacha mkoba wake, na kuingia chumba cha hoteli.

Dola ya Marekani yayumba


Waunda sera kutoka Benki Kuu ya Marekani, wamesema wanafuatilia kilichoko katika uchumi wa taifa, kutokana na kuongezeka kiwango cha riba za benki nchini humo na imefanya thamani ya fedha za dola kushuka.
Mchumi wa nchi hiyo, Gus Faucher, anasema ni hali ya kushangaza kuonekana Dola za Marekani, inashuka thamani hivi sasa
"Nadhani takwimu tulizopata kutoka mkutanoni zinaonyeha vigezo," anasema Faucher, huku wachumi wakieleza shaka yao dhidi ya hali halisi ya sera za Rais mpya, Donald Trump.
Inaelezwa kwamba katika kipindi kifupi kilichopita, tangu Machi mwaka huu, serikali iliongeza kiwango cha riba zake mara tatu.
Pia, katika sura nyingine, inaelezwa kuwa benki zimeendelea kuwa imara katika majukumu yake ya kila siku.
Kwa miaka mingi na katika sehemu nyingi, Dola ya Marekani imekuwa marejeo cha kiwango cha mabadilishano katika fedha za dunia.

Trump:Mkataba wa Paris unalengo la kuiuwa US kiuchumi

Rais Donald Trump ametangaza kujiondoa kwa Marekani katika makubaliano ya Paris juu ya mabadiliko ya tabia nchi uliotiwa saini mwaka 2015.
Amesema mkataba huo si wa haki na unahatarisha mamilioni ya nafasi za kazi za watu wa Marekani.
Kujitoa katika mkataba huo ilikua ni mojawapo ya ajenda wakati wa kampeni za Trump
Bw Trump amesema yuko tayari kuanzisha mashauriano ya mkataba mpya au airejeshe Marekani baadaye katika mkataba huo chini ya masharti yaliyoimarishwa.
Lakini amesema kuwa yeye hawezi kuunga mkono makubaliano ambayo - kwa matamshi yake mwenyewe - yanaadhibu Marekani bila kuwawajibisha wachafuzi wakubwa wa mazingira, ambapo amezitaja China na India.
Bw Trump amesema wakati wa kampeni za urais mwaka jana, aliahidi kwamba angechukua hatua kusaidia sekta za mafuta na makaa yam awe nchini Marekani.
Wapinzani wake wanasema kujiondoa kwenye Mkataba huo ni sawa na Marekani kuyakimbia majukumu yake kama kiongozi katika kukabili changamoto hiyo inayoikabili dunia.
Mkataba wa Paris unaitaka Marekani na nchi nyingine 187 kudhibiti ongezeko la viwango vya joto duniani kuhakikisha kiwango cha joto kinafikia nyuzijoto 2C chini ya kiwango kilichokuwepo kabla ya mageuzi ya kiviwanda, na baadaye kukipunguza zaidi hadi nyuzijoto 1.5C.
Ni Syria na Nicaragua pekee ambazo zilikataa kutia saini mkataba huo.
Akihutubu katika bustani ya White House Rose, Bw Trump amesema mkataba huo wa Paris unalenya kuidhoofisha na kuifanya Marekani kuwa nchi maskini.
Amedai mkataba huo utaigharimu Marekani $3tn ya mapato na nafazi za kazi 6.5 milioni - huku mataifa yanayoshindana na Marekani kama vile China na India yakifaidi.
"Ili kutimiza wajibu wangu wa kuilinda Marekani na raia wake, Marekani itajiondoa kutoka kwa Mkataba wa tabia nchi wa Paris ….lakini itaanza mashauriano ya kujiunga tena na mkataba huo wa Paris au mkataba mwingine mpya kabisa kwa masharti ambayo ni nafuu kwa Marekani," alisema.
Kwenye hotuba yake, alikariri baadhi ya maneno aliyokuwa akiyasema kwenye kampeni.

Griezmann aamua kubaki Madrid

Mshambuliaji Antoine Griezmann ameamua kubaki Atletico Madrid msimu ujao na kumaliza tetesi za kuhamia Manchester United kwa dau la Pauni Milioni 86.
Mpachika mabao huyo wa Kifaransa, kwa kiasi kikubwa amekuwa akihusishwa na kuhamia Old Trafford, lakini baada ya Atletico kufungiwa kusajili wachezaji wapya inaonekana amemaliza tetesi hizo.
Jana jioni kwenye ukurasa wake wa Twitter, Griezmann aliweka picha yake akiwa amevaa jezi ya Atletico ikiwa imeambatana na maelezo yasemayo: "Sasa zaidi kuliko daima#Atleti #WotePamoja'


Thursday, 1 June 2017

ZILIZOCHUKUA NAFASI KATIKA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 02 2017




SIKILIZA KWA MAKINI, TAIFA KWANZA

Hafla ya kuzindua Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa Njia ya kielektroniki

unnamed
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akihutubia baada ya wakati wa kutembelea Kituo cha Kutunzia Taarifa (Data centre) na na  kuzindua Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa Njia ya kielektronini  kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017.
1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akihutubia katika Kituo cha Kutunzia Taarifa (Data centre) wakati wa kuzindua Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa Njia ya kielektronini  kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017.
2
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine akitoka kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua  Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017.
3
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akisalimiana na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika la simu Tanzania TTCL Bw. Waziri Kindamba wakati wa kutembelea Kituo cha Kutunzia Taarifa (Data centre)  na  kuzindua Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa Njia ya kielektronini  kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017.
4
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akisalimiana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Bw. Joseph Kichere wakati wa kutembelea Kituo cha Kutunzia Taarifa (Data centre)  na  kuzindua Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa Njia ya kielektronini  kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017.
5
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akionesha Ipad maalumu aliyopewa ili kumuwezesha  kufuatilia ukusanyaji wa mapato ya kila siku. Kulia kwake ni  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na kushoto kwake ni  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakati wa  kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua  Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017.
6
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein  akionesha Ipad maalumu aliyopewa kumuwezesha  kufuatilia ukusanyaji wa mapato ya kila siku. kushoto kwake ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakati wa  kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua  Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017.
7
 Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akionesha Ipad maalumu itayomuwezesha kufuatilia ukusanyaji wa mapato ya kila siku. Kulia kwake ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein na viongozi wengine wakati wa  kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua  Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017.
8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akishuhudiwa  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine akizindua  Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017.
9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi katika picha ya pamoja na wakuu wa makampuni ya mawasiliano mbalimbali nchini kwenye sherehe ya uzinduzi wa Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017.
10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi katika picha ya pamoja na wakuu wa Mabenki mbalimbali nchini sherehe ya uzinduzi wa Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu

CHADEMA Yaamuru bendera zake kupepea nusu Mringoti

Katibu Mkuu wa Chama hicho Dr Mashinji Leo amezungumza na Waandishibwa Habari Jiji Dar es Salaam.
Dr Mashinji amesema kuwa chama kipo kwenye majonzi makubwa sana baada ya kuondokewa na  mwasisi wa chama hicho mzee Ndesamboro na Chama kimeamua kupeperusha Bendera za chama nusu mringoti nchi nzima.

Uzinduzi wa mfumo wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki

. Rais John Magufuli amesema anajivunia kuwa na mitandao mingi ya simu ambayo inamsaidia kuwasiliana bila kero wakati wowote.
 Amesema hayo leo Juni Mosi, wakati wa uzinduzi wa mfumo wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki.
“Mimi nina mitandao yote ya simu, nina Tigo, Airtel, Vodacom na hata TTCL, mtu akinitafuta huku Airtel,akanikosa ninaweza kuweka Tigo, ili mradi ninatambulika kila mahali,” amesema
 Pia amesema, mitandao hiyo ya simu inamsaidia kupata taarifa mbalimbali zinazoendelea nchini na duniani.
Hata hivyo, Rais amezitaka kampuni za simu kuhakikisha zinalipa kodi ili serikali isikose mapato yake.
Pia Rais amesema hataki kuona taasisi nyingine zinajenga vituo vya ukusanyaji taarifa (Data centre)na badala yake  fedha hizo zitumike kwa ajili ya shughuli nyingine za maendeleo.
 “Data Centre kama hii ni mkombozi mwingine wa kupunguza kero mbalimbali, kwa sababu ukijaza vocha yako uko Zanzibar, ukinunulia vocha yako Kigoma au Moshi, hiyo pesa inakuja TRA, hakuna mabishano” amesema
 Rais amesema hayo leo Juni Mosi, wakati wa uzinduzi wa mfumowa wa serikali wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki ambako pia alitembelea kituo hicho cha ukusanyaji taarifa.

Mionekana ya Watu maarufu katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu

Batuli

 Huu ni mwezi Mtukufu wa Ramadhan, waislamu wote duniani wapo katika mfungo, hapa tumekusogezea picha za muonekano wa mastaa 11 wa Bongo.
 Mr Blue na familia yake
 Nisha
 Jay Moe
 Riyama Ally
Shamsa Ford
 Tunda Man
 Faiza Ally na mwanae
Shetta
 Ommy Dimpoz
Nuh Mziwanda

Man United wakataa kumuuza kipa De Gea

Klabu ya Manchester United imeonyesha imepania kumbakiza kipa wake David De Gea baada ya kukataa kumuuza kwa Real Madrid.
Man United imekataa kitita cha pauni milioni 60 ambayo ingekuwa rekodi ya usajili kwa kipa kutoka katika klabu ya England.
Ingawa hali hiyo imeonyesha kuwashangaza wengi, inawezekana Real Madrid wakarejea na kitita kikubwa zaidi ili kumnasa De Gea ambaye ni raia wa Hispania.
De Gea alitokea katika jiji la Madrid akiwa na Atletico Madrid na kujiunga na Manchester United akiwa kipa kinda.
Lakini kwa misimu miwili mfululizo, amekuwa tegemeo kuu la kikosi cha Man United ambacho kimekuwa kikiyumba.