Tuesday, 8 December 2015

SERIKALI YATOLEA UFAFANUZI WA SIKU YA UHURU



Serikali yatolea ufafanuzi kuhusu Siku ya Uhuru
Picha ni Balozi ombeni sefue akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kusherekea sikukuu ya uhuru kesho

Serikali imeitole ufafanuzi kuhusiana na sikuu ya uhuru ambayo inatafanyika kesho ila kesho sio siku ya mapumziko tofauti na miaka  mingine ya sikukuu hiyo kuwa ya mapumziko katibu mkuu Balozi Ombeni sefue amesema kwa mamalaka aliyonayo Rais kisheria kuwa kesho ni siku ya kazi kama kawaida kwa wale ambao watakuwa na kazi kwa kesho

Kwa upande wa wale ambao hawatakuwa na kazi kesho wametakiwa kufanya usafi katika maeneo wanayokaa kawa kushirikiana na viongozi wa mitaa yao

Aidha Balozi Sefue amesema zoezi la usafi ni la nchi Wananchi washirikiane na viongozi wao katika kufanya usafi katika maeneo wanayowazunguka

imetokana na Rais John Pombe Magufuli kutangaza kuwa ifikapo Disemba 09-11-2015 kuwa itakuwa ni siku ya kufanya usafi katika maeneo yetu yanayotuzunguka na hakutakuwa na sherehe ya kusherekea Uhuru Badala yake ni kufanya usafi.


MNIGERIA WA YANGA SC KUTUA LEO USIKU



Na kalonga kasati
Kiungo wa kimataifa  wa niger issoufou bobacar garba sasa anatarajiwa kuwasili  leo usiku kwa majaribio ya wiki moja ya kocha Hans van der pluijm kutoa uamuzi awali garba ilikuwa awasili jana usiku lakini alichelewa kuunganisha ndege mijini Addis  abba Ethiopia
 Na kulazimika kulala hadi leo

Dirisha dogo la usajili wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara imefungwa disemba 15 na kweli  mholanzi pluijm aliyependekeza mchezaji huyo atakuwa na wiki moja tu ya kutoa majaribu juu ya mnigeria huyo aliyezaliwa februari 2 mwaka 1990 taarifa zinasema garba kwa sasa anacheza kwao baada ya kuondoka Tunisia ingwa hakupata nafasi ya kucheza ingwa yeye anasema ni hila visa si sababu ya uwezo 

Katika wasifu wake garba anatambulishwa kama kiungo lakini yanga wanasema wanaleta mshambuliaji
Na huyu atakuwa mchezaji wa pili kuletwa na kocha pluijm baada wa kwanza Joseph Zuttah ambaye hata hivyo aliachwa baada ya mechi saba
Garba aliyezaliwa mji waNiamey mwenye urefu wa futi 5 na nchi 6 kisoka alianzia klabu ya As fan ya kwao 2010 kabla ya kuhamia Thailand  ambako alichezea klab za Muangthong united mwaka 2011 na Phuket  mwaka 2012 alitua  club ya African ya Tunisia  ambako hakucheza mechi hadi anasimamishwa

Es Hammam ambako pia hakucheza  wasifu wake unaonyesha tangu ameondoka Es Hammam-Sousse hajapata timu nyingine lakini uongozi wa yanga sc umejiridhisha anacheza bingwa ya kwao As Douanes

Mwenyekiti wa yanga sc Yusuph manji ametoa agizo la kutosajiliwa mchezaji yoyote kutoka Uganda Kenya hata awe anaweza kucheza kama christiano Ronaldo itakuwa kazi bure

Vijana wametakiwa kushiriki kesho katika kufanya usafi



Na Kalonga kasati
Umoja wa vijana wa chama chama cha mapinduzi mkoa wa kigoma(UVCCM)wamefanya usafi katika hospitali ya mkoa maweni sambamba na kuwafariji wagonjwa waliolazwa katika wodi mbalimbali hospitalini hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa  mbunge wa viti maalum kupitia umoja huo wa vijana Zainabu Katimba alisema kuwa wameamua kuwafariji wagonjwa na kufanya usafi hospitalini hapo ili kuendana na kasi yam he Rais john pombe magufuli  wa hapa kazi tu.

Sisi kama vijana tumeamua kusherekea kauli mbiu ya mhe Rais magufuli  ya hapa kazi tu kwa vitendo hii si kwa ajili ya siku ya uhuru tu kesho hili ni zoezi endelevu tutakuwa tunalifanya mara kwa mara alisema Bi Katimba.
Aliwataka wananchi wote bila kujali itikadi zao kumuunga mkono Mhe Rais kwa kujitokeza siku ya kesho na kufanya usafi katika maeneo yao kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kuepekana na maradhi  ya milipuko  kama kipindupindu na mengine.

Naye Mwenyekiti wa umoja wa vijana (uvccm) mkoa Peter Msanjile alisema kuwa na zoezi hilo la usafi katika maeneo mbalimbali linatekelezwa  na vijana katika mikoa yote
Msanjile amempongeza Rais wa awamu ya tano John pombe magufuli kwa kazi nzuri anazofanya kwa kuwajibisha wahujumu uchumi

Monday, 7 December 2015

RAIS MAGUFULI AMEVUNJA BODI YA BANDARI NA KUMFUKUZA KAZI KATIBU MKUU WA WIZARA YA UCHUKUZI



Na Kalonga kasati
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania John pombe magufuli amevunja bodi ya bandari nchini pamoja na kutengua uteuzi wa katibu mkuu wa wizara ya uchukuzi Dk Shabani Mwinjaka pamoja na  Mkurugenzi mkuu wa bandari Awadhi massawe  na mwenyekiti wa bodi ya bandari Profesa Joseph msambichaka
Kuvunjwa kwa bodi hiyo kumetokana na uendaji mbovu wa mamlaka hiyo kwa muda mrefu na kitendo cha kutokuchua hatua za haraka katika vyanzo husika.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake waziri mkuu Kassim majaliwa ofisini kwake leo jijini Dar es salaam amesema kutenguliwa kwa uteuzi huo kutokana na ziara alizofanya bandari ya Dar es salaam  na kubaini kuwepo na mianya ya ukwepaji wa kodi ikiwemo makontena 2387 yaliyopitishwa kati ya machi na septemba mwaka jana.
Amesema upotevu huo kutokana na mfumo wa kupokelea malipo ambao unatoa mwanya wa kupoteza mapato ya serikali kutaka mfumo huo ubadilishwe kufikia desemba 11.
Waziri mkuu kassim majaliwa amesema kuwa kutokana na utendaji wa bandari huo mbovu iliwataja majina ya wahusika na upitishaji wa makontena hayo bila ya kuwepo na taarifa yoyote hivyo amewasimamisha kazi wasimamizi 8 wa bandari kavu (icd) ambao ni Happy god Naftari juma Prosper kimaro mkango ali John Elisante na James Kamwomwa.
Wengine ambao hakuwepo kwenye ripoti hiyo ni viongozi wa sekta zilizotoa ruhusa makontena kutoka ndani ya bandari wahusika wakuu hao ni Shaban mngazija aliyekuwa meneja mapato Rajab  mdoe Mkurugenzi wa fedha  na mkuu wa bandari kavu ibin masoud kaimu mkurugenzi wa fedha Apolonia mosha meneja wa bandari msaidizi wa fedha



Na kalonga kasati
Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma nchini ambao ulizinduliwa agosti mwaka huu
Akiongea na vyombo vya habari leo katibu mkuu Hab mkwizu amesema utekelezaji huo umeanza rasmi disemba 2015 ambapo kila mtumishi wa ummaataweka saini ya kiapo kwa kuzingatia taratibu zilozoweka na mazingira ya taasisi husika
Utaratibu wa utekelezaji wa ahadi ya uadilifu kwa utumishi wa umma umetolewa kupitia waraka wa mkuu wa utumishi wa umma  wa mwaka 2015 kuhusu utekelezaji wa ahadi ya uadilifu kwa viongozi watumishi wa umma wa sekta binafsi wa tarehe 1 agosti 2015 alisema mkwizu.
Mkwizu aliongezea kwa kusema uanzilishwaji wa uadilifu ni mwendelezo wa uundaji wa vyombo vya kusimamia maadili baada ya ongezeko kubwa la ubadhirifu utoro sehemu za kazi kushuka kwa nidhamu katika kipindi cha miaka ya thelathini na tisini
Alivitaja vyombo vipengele ambavyo vilianzishwa kusimamia ahadi kuwa ni sektarieti ya maadili ya viongozi wa umma tume ya haki binadamu na utawala bora na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU)
Aidha Mkwizu amtoa kwa waajiri wote kuhakikisha kuwa utekelezaji wa ahadi ya uadilifu unakamilika ifikapo tarehe 31-12-2015 na utekelezaji wakekwa kila ifikapo juni 30 ya kila mwaka fomu ya ahadi ya uadilifu zinapatikana katika tovuti ya Rais.

Monday, 19 October 2015

INCREASE YOUR INCOME PER MONTHLY

Je kipato chako ni kidogo, akitosherezi mahitaji yako, je wewe ni mwanafunzi na unahitaji kupata kipato kisicho haribu mwenendo na ratiba zako za masomo? Tatua tatizo la kipato kwa kutumia mtandao/ internet ni rahisi unachotakiwa kufanya temblea tofuti hii na ujiregister http://jobrize.com/index.php?ref=648278 ni bure hamna malipo yoyote enjoy your monthly addition salaries!

Tuesday, 13 October 2015

Aliyemteka Ulimboka huyu hapa

Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Rashid Othman
RAMADHANI Ighondu, afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), ndiye ametajwa kuwa mtekelezaji wa mkakati wa utekaji wa Dk. Steven Ulimboka, MwanaHALISI limegundua.
Afisa huyo, licha ya kutambuliwa na Dk. Ulimboka mwenyewe, ndiye simu yake ilitumika kuandaa kikao ambako daktari alitekwa.