Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi katika mradi wa
ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3) katika Wilaya ya Maswa
mkoani Simiyu. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony
Mtaka watatu kutoka kulia Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa
wakwanza kulia pamoja na viongozi wengine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengiene akikata
utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa
mradi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya mradi wa ujenzi
wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3) kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu
wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Cristianus Ako kabla ya
kuweka jiwe la msingi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Maswa kabla ya
kuweka jiwe la msingi ujenzi wa wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3),
mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mkuu wa mkoa wa Simiyu
Antony Mtaka mara baada ya kuwasili Wilayani Maswa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi
Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kuwasili Wilayani Maswa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa
TAMISEMi na Kazi maalumu kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Haji
Omari Heri kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara hiyo ya
Mwigumbi-Maswa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Waziri wa TAMISEMi na
Kazi maalumu kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Haji Omari Heri
wakimwagilia maji mti mara baada ya kuupanda baada ya uwekaji wa jiwe la
msingi ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3), mkoani Simiyu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini kwenye Ubao kwa kutumia
Chaki zinazotengenezwa na Kiwanda cha Chaki cha Maswa Mkoani Simiyu.
Rais Dkt. Magufuli aliwapongeza wenye kiwanda hicho na kuwashauri
kukipanua zaidi ili kiweze kuwafikia Watanzania wengi wenye mahitaji ya
Chaki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wakazi wa Maganzo mkoani
Shinyanga mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wakazi mbalimbali wa Maswa
mara baada ya kumaliza kuwahutubia Wilayani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony
Mtaka wakiangalia utengenezwaji wa Chaki katika kiwanda cha Chaki cha
Maswa mkoani Simiyu.
PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment