Haya ndo maneno aliyoweka Zito Kabwe kwenye ukurasa wake wa facebook
Kwanini Viongozi hudanganya?
Miaka michache iliyopita nilisoma kitabu kimoja kiitwacho WHY LEADERS
LIE. Mwandishi wa kitabu hicho anaitwa John Mearsheimer. Anasema maRais
husema uwongo kwa sababu huona jambo zuri kwa wananchi wao.
Hata hivyo huwezi kudanganya watu wote kwa muda wote. Unaweza kudanganya watu wachache kwa muda Fulani.
Leo Rais wetu mtukufu mpenda kusema ukweli maana msema kweli mpenzi wa
mungu alikuwa huko Bariadi na kuzungumza na wananchi. Katika mazungumzo
yake kasema hakuna hatari ya njaa nchini na kwamba wanasiasa na magazeti
yaliyoandika kuhusu njaa wanalipwa na Wafanyabiashara wenye tani 25,000
za Mahindi bandarini. Rais wetu mtukufu anasema mahindi hayo wenye nayo
wanataka yaingie nchini bila kulipa kodi, yapewe msamaha Wa kodi.
Akasema mahindi hayo yametoka Brazil na ni mabovu hayafai kwa matumizi
ya binaadamu. Akamalizia kwa kusema kuwa hataruhusu mahindi hayo Yaingie
nchini mpaka yalipiwe kodi.
Rais wetu mtukufu anajua kuwa mahindi mabovu hayapaswi kuingizwa nchini
hata Kama yakilipiwa kodi kwa sababu ni mabovu. Yanapaswa kuharibiwa na
TFDA ( mamlaka ya chakula na dawa).
Rais pia amekuwa Waziri muda mrefu na anajua kuwa Tanzania kuna kitu
kinaitwa pre-shipment inspection ambapo bidhaa zinazoingizwa nchini
hukaguliwa huko huko zinapotoka kabla ya kuruhusiwa kupakiwa kwenye
meli. Hayo mahindi mabovu yameingiaje nchini?
Rais wetu mtukufu msema Kweli mpenzi wa mungu mbona anakuwa inconsistent
katika hotuba moja ndani muda mfupi? Kwa wataalamu wa saikolojia majibu
wanajua. Kuna kitu Rais anaficha. Nacho ni kwamba Serikali yake
ililibishia Bunge kuhusu Bajeti ya kununua chakula NFRA. Mwaka huu
Serikali haikununua chakula cha akiba Ndio maana wananchi wanapata Tabu.
Hivi Serikali ina majibu ya RC wa Arusha kuhusu vibali alivyokamata vya kuuza mahindi Kenya kipindi Hiki?
Kwanini Kiongozi useme uwongo Kwa wananchi wako? Ili iwe nini? Kwanini usikiri makosa? Wakosoaji wako ndio wanaokusaidia.
No comments:
Post a Comment