Tuesday, 10 January 2017

Yanga kuwakosa Tambwe, Chirwa, Zulu na Ngoma leo dhidi ya Simba

  Image result for LWANDAMILA
Kochawa Yanga, Mzambia George Lwandamina amesema kwamba ataingia kwenye mchezo wa leo dhidi ya mahasimu, Simba hali ya kikosi chake ikiwa si nzuri sana.
Lwandamina amesema kwamba wachezaji wake wanne tegemeo wote ni majeruhi na hawawezi kucheza leo.
Lwandamina amewataja wachezaji majeruhi ni Wazambia wenzake, viungo Justin Zulu na Obrey Chirwa na washambuliaji Mrundi Amissi Tambwe na Mzimbabwe Donald Ngoma.
George Lwandamina amesema wachezaji wake tegemeo wanne ni majeruhi kuelekea mchezo wa leo
Pamoja na hao, Lwandamina alisema beki Pato Ngonyani na mshambuliaji Matheo Anthony nao wote ni wagonjwa na hawana uhakika wa kucheza kesho.

Kwa ujumla Lwandamina ambaye timu yake ilifungwa 4-0 na Azam FC Jumamosi kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi A, alisema ataingia kwenye mchezo wa kesho katika mazingira magumu ya kukatisha tamaa.

“Lakini hatuna namna nyingine, lazima tuingize timu tukapambane,”alisema. Yanga inakutana na mahasimu, Simba katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku wa leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

No comments:

Post a Comment