Tuesday, 10 January 2017

Ujumbe wa Trump kwa shirika la Toyota kupitia mtandao wa Twitter

Ujumbe wa Trump kwa shirika la Toyota katika mtandao wa Twitter
Trump aandika ujumbe katika mtandao wa Twitter na kusema kuwa ataliongezea ushuru Shirika la Toyota endapo litaendelea na mpango wake wa kufungua tawi nchini Mexico.
Trump amekuwa akitoa vitisho kwa makampuni tofauti nchini Marekani na kutaka uwekezaji wote ufanywe nchini humo.
Msemaji wa shirika la Toyota amesema anashangazwa na matamshi ya rais mteule Donald Trump ya kutaka tawi la Mexico lisianzishwe.

"Tumekuwa tukifanya kazi Marekani kwa muda mrefu sana na shirika letu halidhani kama uanzishaji wa tawi letu nchini Mexico litaathiri ajira kwa raia wa Marekani kwa namna yoyote ile" alisema msemaji huyo.
Hata hivyo vitisho vya Trump ndivyo vilisababisha shirika la Ford kuacha kutengeneza magari Mexico.

No comments:

Post a Comment