Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikagua sehemu ya kuhifadhia mizigo ya
abiria kilivyoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo( jana) katika
Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere ,kulia ni
Mkurugenzi wa Uwanja huo Bw. Paul Rwegasha.
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha akimuonesha
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa chumba cha
kuhifadhia mizigo ya abiria kilivyoteketea kwa moto usiku wa kuamkia
leo (jana).
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha akimuonesha
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa chumba cha
kuhifadhia mizigo ya abiria kilivyoteketea kwa moto usiku wa kuamkia
leo (jana).
PICS 4: Mkurugenzi wa Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha
akimuonesha Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame
Mbarawa chumba cha kuhifadhia mizigo ya abiria kilivyoteketea kwa moto
usiku wa kuamkia leo (jana).
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa wanahabari
(hawapo pichani) mara baada ya kukagua chumba cha kuhifadhia abiria
kilichoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo (jana),wa kwanza kulia ni
Kaimu Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Bw. Gabriel Migire. (Picha na
Benjamin Sawe-Maelezo).
Serikali imesema imeunda Tume ya
uchunguzi ya watu 12 ili kuweza kuchunguza na kubaini chanzo cha ajali
ya moto iliyotokea jana saa Tano usiku katika chumba kidogo cha
kuhifadhia mizigo kilichopo kwenye jengo la Pili la abiria (Terminal II)
katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es salaam leo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa Tume hiyo iliyoundwa inaongozwa na
Joseph Nyahende ambae anatoka katika ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege nchini.
“Ninategemea kupata ripoti ya
kitaalamu kutoka kwa Tume hii, ili kutusaidia kubaini kiundani juu ya
chanzo haswa kilichopelekea moto huu”, amesema Waziri Mbarawa.
Aidha, Waziri Mbarawa amefafanua
kuwa huduma katika jengo hilo zinaendelea kama kawaida ambapo awali
zilisitishwa na kuhamishiwa katika Jengo la Kwanza la abiria (Terminal
I).
“Mara baada ya moto kutokea, kitu
cha kwanza kilichofanyika ni kuudhibiti moto huu ili usiweze kusambaa
katika maeneo ambayo hayajaathirika, kisha tukatafuta njia za kurudisha
huduma kwa abairia”, amesisitiza Profesa Mbarawa.
Katika hatua nyingine, Profesa
Mbarawa ameipa miezi miwili kampuni ya mizigo ya Swissport kurekebisha
huduma zinazolalamikiwa na wateja wake na endapo itashindwa hatua za
kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Uwanja wa Ndege wa JNIA, Paul Rwegasha ameeleza kuwa tathmini na gharama
za mizigo iliyokuwa imehifadhiwa katika chumba hicho bado haijajukana,
ambapo ripoti itaeleza gharama hizo pindi itakapokamilisha uchunguzi
wake.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment