Katibu Mkuu wa Chama cha
Tanzania-China Friendship Promotion Association Bw.Joseph kahama
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya matembezi ya
kupinga ujangili wa Tembo (Walk for Elephant 2017) yatakayofanyika kesho
asubuhi kuanzia saa 12 asubuhi kuanzia Ubalozi wa China mpaka Hoteli ya
Sea Cliff.Kushoto kwake ni Hongxiang Huang kutoa China House.
Katibu Mkuu wa Chama cha
Tanzania-China Friendship Promotion Association Bw.Joseph kahama
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya matembezi ya
kupinga ujangili wa Tembo (Walk for Elephant 2017) yatakayofanyika kesho
asubuhi kuanzia saa 12 asubuhi kuanzia Ubalozi wa China mpaka Hoteli ya
Sea Cliff.
Katibu Mkuu wa Chama cha
Tanzania-China Friendship Promotion Association Bw.Joseph kahama
akionyesha tangazo lenye ujumbe wa kuhimiza matembezi ya ku kupinga
ujangili wa Tembo (Walk for Elephant 2017) yatakayofanyika kesho asubuhi
kuanzia saa 12 asubuhi kuanzia Ubalozi wa China mpaka Hoteli ya Sea
Cliff. Kushoto kwake ni Hongxiang Huang kutoa China House.
Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.
Na Frank Shija-MAELEZO.
Mkapa kuongoza matembezi ya hiari ya kilomita tano yanayojulikana kama Walk for Elephant Dar es Salaam 2017yatayofanyika kesho kuanzaia saa 12 asubuhi yaikianzia Ubalozi wa China hadi Sea Cliff Hotel.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu
wa Chama cha Urafiki baina ya Tanzania na China (TCFPA) Joseph Kahama
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na matembezi hayo
leo jijini Dar es Salaam.
Kahama amesema kuwa yana lengo la kuonyesha umoja katika kupinga ujangili unaofanywa dhidi ya Tembo.
“Tunatarajia kuwa na matembezi ya
kwa ajili ya kupinga ujangili dhidi ya Tembo ambapo wageni wetu
mashuhuri wanatarajiwa kuwa Marais wastaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi na
Mzee Mkapa atakayepokea matembezi hayo katika Hotel ya Sea Cliff,”
alisema Kahama.
Aliongeza kuwa zaidi ya watu 550
wamethibitisha kushiriki katika matembezi hayo wakiwemo baadhi ya watu
maarufu kama vile Jokate Mwigelo, Mrisho Mpoto na wasanii wengine.
Aidha Katibu Mkuu huyo alisema
kuwa Chama cha Urafiki baina ya Tanzania na China(TCFPA) imeanzishwa kwa
nia ya kudumisha urafiki na uhusiano baina ya raia wa nchini hizo
mbili.
Akijibu swali la mwandishi wa
habari aliyetaka kujua ni kwanin china imeamua kusaidia katika vita
dhidi ya ujangili ili hali inatajwa kuwa miongoni mwa soko kubwa la
bidhaa za meno ya Tembo, Kahama alisema kuwa Serikali ya China haiku
tayari kuona nchi yake inatajwa kama soko la meno ya Tembo ndiyo maana
Rais Xi Jinping wa China na Barrack Obama wa Marekani wamewahi kutoa
tamko la pamoja la kupinga ujangili na ni kosa la jina kwa rai wa China
kukamatwa na nyara hizo.
Chama hicho kimekusudia kuifanya
tarehe 14 mwezi wa kwanza kila mwaka kuwa siku ya matembezi ya Walk for
Elphant Dar es Salaam 2017 ili kujenga utamaduni endelevu wa kupinga
ujangili.
No comments:
Post a Comment