Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump anatarajiwa kuapishwa January 20
2017, ushindi wa Donald Trump umetajwa kuwa wa kihistoria katika siasa
za Marekani.
Wakati zikiwa zimebaki siku 10 Trump kuapishwa kitu cha kufahamu ni
kwamba Trump anaiweka rekodi ya kuingia White House akiwa na umri mkubwa
zaidi.
Trump ataapishwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani akiwa na umri wa miaka 70,
rekodi hiyo ilishikiliwa na Ronald Reagan ambaye aliingia White House
akiwa na miaka 69 mwaka 1981.
Rais wa zamani wa Marekani, Theodore Roosevelt ndiye Rais aliyeingia
madarakani akiwa na umri mdogo zaidi, Roosevelt alikuwa na miaka 42,
John F. Kennedy alikuwa mkubwa kidogo alipochukua madaraka miaka 60
baadaye akiwa na umri wa miaka 43.

No comments:
Post a Comment