Na Daudi Manongi-MAELEZO
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri
Mkuu,Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Mamlaka ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi – VETA wanaendesha mpango wa kutathmini
na kurasimisha ujuzi uliopatikana nje ya Mfumo rasmi wa Mafunzo.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Katibu
Mkuu wa Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Eric Shitindi, imesema kuwa
mpango huo unatoa fursa ya kufanyiwa tathmini ya ujuzi, kupewa mafunzo,
kuziba upungufu na kisha kutunukiwa cheti.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa sifa
za mwombaji wa mafunzo hayo ni pamoja na uzoefu usiopungua miaka mitano
na umri usiozidi miaka 45.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa
fani mbalimbali zitakazohusika ni Uashi, Useremala, Ufundi Magari
(makenika), upishi, uhudumu wa hoteli, Bar na Migahawa.
Ili kufanya maombi waombaji
wanatakiwa kufika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa, Mji au Wilaya
iliyoko karibu ili kuchukua fomu za kujaza maombi bila malipo yeyote na
maombi hayo kuwasilishwa kuanzia tarehe 5 hadi 25 Januari 2017.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa
mchakato wote wa tathmini na urasimishaji wa ujuzi utagharamiwa na
Serikali na pia watakaokidhi sifa, vigezo na masharti watajulishwa kwa
ajili ya usaili kuanzia Tarehe 10 Februari 2017.
No comments:
Post a Comment