Sunday, 15 January 2017

Habari Picha

KIG1
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala, akimkabidhi Bi. Salma Salum kadi ya bima ya Afya katika viwanja vya Mnarani, Mwembe Kisonge, Mjini Unguja, Zanzibar. Kadi zaidi ya 200 walikabidhiwa wazee wa Jimbo la Kikwajuni ambapo anatoka Mbunge wa Jimbo hilo ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto). Picha zote na Felix Mwagara
KIG2
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala, katika Sherehe za Kukabidhi Bima ya Afya kwa Wazee wa Jimbo la Kikwajuni, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnarani, Mwembe Kisonge, Mjini Unguja, Zanzibar.  Picha na Felix Mwagara.
KIG3
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kikwajuni (hawapo pichani), kabla ya kukabidhi kadi za Bima ya Afya kwa wazee zaidi ya 200 wa jimbo hilo ambalo anatoka Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto). Kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor Salim Jazeera.  Tukio hilo lilifanyika katika Viwanja vya Mnarani, Mwembe Kisonge, Mjini Unguja, Zanzibar.  Picha na Felix Mwagara.
KIG4
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akuzungumza na wananchi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala (wapili kulia), kukabidhi kadi za Bima ya Afya kwa Wazee zaidi ya 200 wa Jimbo la Kikwajuni. Kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo,  Nassor Salum Jazeera. Tukio hilo lilifanyika katika Viwanja vya Mnarani, Mwembe Kisonge, Mjini Unguja, Zanzibar.  Picha na Felix Mwagara.
KIG5
Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapindiuzi, Zanzibar, Bi Harusi Said akizungumza na wananchi katika Sherehe za kukabidhi Bima ya Afya kwa Wazee zaidi ya 200 wa Jimbo la Kikwajuni ambapo anatoka Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) ambaye ni Mbunge wa  Jimbo hilo.   Tukio hilo lilifanyika katika viwanja vya Mnarani, Mwembe Kisonge, Mjini Unguja, Zanzibar.  Picha na Felix Mwagara.

No comments:

Post a Comment