Sunday, 15 January 2017

Habari katika picha

UCO
Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila (wa kwanza kulia) pamoja na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika kivuko cha kuelekea katika Wilaya ya Ukerewe, Mwanza kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme jua inayotekelezwa na kampuni ya Rex Energy.
UCO 1
Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji   kutoka kampuni ya Rex Energy, Francis Kibhisa (kulia) katika ziara hiyo.
UCO 2
Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila (kulia) akibadilishana mawazo na Afisa Sheria kutoka  Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Peter Malendecha (kushoto) mara baada ya kuwasili katika wilaya hiyo.
UCO 3
Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila (kulia nyuma) pamoja na wajumbe  wengine wakielekea katika kisiwa kidogo cha Ghana/Siza kwa ajili  ya kukagua miradi ya umeme jua inayotekelezwa na kampuni ya Rex Energy.
UCO 4
Mkurugenzi Mtendaji   kutoka kampuni ya Rex Energy, Francis Kibhisa (kulia) akielezea hatua ya utekelezaji ya miradi ya kusambaza umeme katika kisiwa cha Ghana/Siza wilayani Ukerewe  kwa Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila (kushoto)
Sehemu ya miundombinu ya umeme iliyokamilika katika kisiwa cha Ghana/Siza
UCO 5UCO 6
Katibu wa Kitongoji cha Ghana/Siza  wilayani Ukerewe, Frank Matondane akielezea mahitaji  ya umeme katika kitongoji hicho mbele ya Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila pamoja na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini (hawapo pichani)
UCO 7
Mkurugenzi Mtendaji   kutoka kampuni ya Rex Energy, Francis Kibhisa (kushoto) akionesha eneo litakalowekwa mitambo ya umeme  katika kitongoji cha  Ghana/Siza wilayani Ukerewe kwa Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila (kulia).

No comments:

Post a Comment