Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kupitia baraza la wafugaji tarafa na
Ngorongoro imeanza kusafirisha shehena ya mahindi kwa wakazi wa
Ngorongoro kutoka ghala la taifa la chakula ili kutatua tatizo la njaa
linalowakabili zaidi ya watu elfu themanini wanaoishi ndani ya mamlaka
hiyo ambapo kwa awamu ya kwanza imetoa tani mia tisa zitakazo sambazwa
kwenye kaya elfu ishirini.
Akizungumza katika zoezi la kupakia mahindi hayo mwenyekiti wa bazara
la wafugaji Ngorongoro Edward Maura amesema mkataba waliyoingia ni
kununua zaidi ya tani elfu tatu kwaajili ya wakazi hao kuepuka ghalama
za wananchi kuuziwa gunia moja la mahindi kwa shilingi lakimoja kutoka
kwa walanguzi wakati hawana fedha.
Mwenyekiti wa kamati ya lishe na usalama wa chakula kutoka baraza la
wafugaji Ngorongoro Godfrey Lenia amesema mkataba huo ni wa miaka
mitano ambapo kila robo ya mwaka wananchi watapatiwa gunia elfu kumi na
nane za mahindi sawa na tani miatisa kwa ajili ya watu wanaosumbuliwa
kwa njaa ndani ya hifadhi hiyo.
Awali wakisaini mkataba wa kunua mahindi na ghala la taifa la chakula
mhifadhi mkuu wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro redy Manongi amesema
serikali kupitia mamlaka ya Ngorongoro itaendelea kutoa chakula kwa
wakazi hao ili kuimaRisha uhifadhi kwakuwa hawaruhusiwi kulima ndani ya
hifadhi hiyo.
No comments:
Post a Comment