Bendera ya Cuba ikipepea nusu mlingoti, na mitaa ikiwa mitupu
Kundi maarufu linaloipinga serikali ya Cuba limesitisha maandamano yake
ya kila wiki kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka kumi na tatu
kufuatia kifo cha Fidel Castro ambaye wao wamekuwa wakimpinga kwa miaka
yote.Kiongozi wa kundi hilo la wanawake maarufu kama Ladies in White, Berta Soler, amesema ametaka kutoa fursa kwa wengine kuomboleza na hivyo hatasheherekea kifo cha mtu yeyote.
Maandamano hayo ya wanawake ya kila wiki ni kwa lengo la kuwaunga mkono waume zao waliofungwa kwa sababu ya kuipinga serikali.
Kumekuwa na hali ya simanzi katika mji mkuu wa Havana siku kilipotangazwa kifo cha Fidel Castro. Mwandishi wa BBC mjini humo amesema watu bado wapo katika mshtuko.
Baadhi ya raia mjini Havana wanasema wameanza kukubaliana na hali halisi:
Lazaro Alonso, anasema " Ni vigumu sana kukubali, lakini ndivyo maisha yalivyo. Tunaendelea kufanya kazi kwa bidii, kusonga mbele, hakuna kitakachozuia huo mchakato, na tunatahadhari kwamba ndio, iko siku mambo makubwa yatatokea nchini humu."
Victor Manuel, naye amenukuliwa akisema "kwetu sisi, kamanda wetu ndio baba wa familia, baba wa mapinduzi, baba tuliyekuwa nae, ambae siku zote na leo tunahisi tumempoteza katika maisha yetu."
Leo Jumatatu, Cuba inaanza siku tisa za maombolezo rasmi.
No comments:
Post a Comment