Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na Mmiliki wa Wasafi
Classic Msanii Naseeb Abdul (Diamond Platinumz) wakati alipotembelea
Studio za Wasafi Classic kujionea utendaji kazi wa studio hiyo Novemba
23,2016.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na
Mmiliki wa Wasafi Classic Msanii Naseeb Abdul (Diamond Platinumz) na wasanii harmonize na Rich Mavoko.
Na Mwandishi Wetu.
Kundi la Muziki wa kizazi
kipya(Bongo Flavour) Wasafi limemuomba Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye kusaidia wasanii wa muziki huo
kujivunia kazi yao kwa kupata maslahi ya kazi hiyo kwa maendeleo yao na
taifa kwa ujumla.
Akizungumza wakati Waziri huyo
alipotembelea Studio za Wasafi na kujionea utendaji kazi wa studio hiyo,
Mmiliki wa studio hizo Naseeb Abdul (Diamond Platinumz) amesema,
kumekuwa na changamoto nyingi katika tasnia ya muziki hasa wizi wa kazi
zao ambazo zimekuwa zikirudufiwa na kuuzwa kiholela ndani na nje ya nchi
bila wao kufaidika na uuzwaji wa kazi hizo.
Changamoto nyingine alizozitaja
msanii Diamond ni pamoja na kupunjwa mapato yatokanayo na Miito ya Simu
(Caller tunes) , kukosekana kwa ukumbi wa kisasa kwa ajj ili ya
kufanyia maonesho makubwa ya muziki nchini, kuongezeka kwa uwiano wa
nyimbo za kitanzania zinazopigwa redioni dhidi ya nyimbo za kigeni hasa
kutoka Afrika ya Magharibi.
Aidha wamemuomba Waziri Nape
Moses Nnauye kuwasaidia kupata Elimu juu ya ulipaji kodi ili tasnia ya
Muziki nayo iweze kuwa kati ya tasnia zenye mchango mkubwa kwa pato la
taifa kwa maendeleo ya wasanii na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amehaidi kuzifanyia
kazi changamoto hizo na kuifanya tasnia ya muziki kuwa ajira kubwa kwa
vijana wengi kwa kuongeza vipato vyao na pato la taifa kwa ujumla.
Wasafi Classic ni kundi la Muziki
wa kizazi kipya(Bongo Flavour) Tanzania linalomilikiwa na Msanii Naseeb
Abdul (Diamond Platinumz) na mpaka sasa lina wasanii wapatao 16 na
linaongozwa na mameneja Babu Tale, Said Fella na Sallam SK.
No comments:
Post a Comment