Maisha ya Fidel Castro enzi za uhai wake
Picha za maisha ya Amri jeshi mkuu Fidel Castro,aliyeongoza mapinduzi ya kikomunisti na kuiongoza Cuba kwa miaka 50
Fidel Castro alizaliwa mwaka wa 1926, azaliwa mkoa wa kaskazini
mashariki wa oriente nchini Cuba na tajiri wa ukuzaji wa miwa. Alijiunga
na siasa za mapinduzi akiwa na umri mdogo
Baada ya miaka miwili jela kwa kuongoza mapinduzi yaiyotibuka, alienda
mafichono nchini Mexico. Mwaka 1956 alirudi na chama chake cha mapinduzi
kikaongoza.Castro mwishowe akapata mamlaka ya kuiongoza Cuba tarehe
1,mwaka 1959,kama waziri mkuu kwa kumshinda Fulgencio Batista
Mwaka 1961,Castrol aliongoza kikosi chake cha jeshi dhidi ya raia wa
Cuba 1,500 waliokuwa uhamishoni. waliohamishwa walikuwa wanafadhiliwa na
CIA, walivamia Bay of Pigs ili kuishinda serikali yake
Alipata majaribio kubwa mwaka 1962 , pale rais wa Marekani John Kennedy alipomuonya kuondoa makombora yake kutoka cuba
Mwishowe,viongozi Nikita Khrushchev na Castro waliondoa makombora na tishio la vita vya nyuklia vikazuiwa
Amri jeshi mkuu huyo alipenda kushiriki mchezo wa baseball. Hapa
anaonekana akicheza katika chuo cha ualimu huko Sierra Maestra mwaka wa
1962.
Wacuba wengi walimchukulia kama dikteta wa ukandamizaji
Mamia ya raia wa Cuba walikimbia makwao,kuelekea Marekani,kwa kutumia maboti yaliokuwa hatari
Lakini Fidel Castrol alipata uungwaji mkono kuwa miongoni mwa viongozi waliohudumu kwa miaka mingi duniani
Baada ya kufanyiwa upasuaji wa utumbo, alimkabidhi rasmi madaraka ya
urais kakake Raul.Alioneka mara chache,kabla ya kung’atuka madarakani
mwezi Februari mwaka 2008
Mwezi Septemba, Fidel Castrol alihutubia umma kwa mara ya kwanza baada
ya miaka minne. Hotuba yake ilikuwa ya kwanza tangu mwezi Julai mwaka
2010 alipotoka kufanyiwa upasuaji wa utumbo. Alionekana kwa umma
alipokuwa akisherehekea mwaka wa 90 wa kuzaliwa kwake mwezi Agosti
No comments:
Post a Comment