Kwa mujibu wa mtandao wa Goal, Bruce Arena ndiye anayetajwa kuwa kocha
mpya wa timu ya taifa ya Marekani kufuatia kutimuliwa kwa Jurgen
Klinsmann.
'
Arena, ambaye alikuwa kocha wa taifa hilo kwenye World Cup ya mwaka 2002
na 2006, ataachana na waajiri wake wa sasa LA Galaxy na kurithi mikoba
ya Jurgen Klinsmann. Taarifa rasmi inatarajiwa kutolewa leo.
Marekani wameamua kuachana na Klinsmann kufuatia matokeo mfululizo
yasiyoridhisha katika michezo ya hatua ya kufuzu fainali za Kombe la
Dunia mwaka 2018 nchini Russia.
Kufuatia kupoteza michezo miwili mfululizo ya kufuzu fainali za Kombe la
Dunia, ikiwemo mchezo wa nyumbani dhidi ya Mexico na ule wa kipigo cha
4-0 kutoka kwa Costa Rica, maafisa wa Soka Marekani wameamua kusitisha
mkataba wake ambao ulikuwa ufikie kikomo mwaka 2018 baada ya Michuano ya
Kombe la Dunia.
Arena (65), ambaye ameshinda mataji matano ya MLS akiwa na Galaxy na
D.C. United, hivi karibuni alisaini mkataba mpya wa miaka miwili wa
kuendelea kuifundisha LA Galaxy. Hata hivyo ni vigumu sana kwa kocha
huyo kukataa ofa ya kulinoa taifa hilo na kuendelea kubaki Galaxy.
No comments:
Post a Comment