Mchezaji wa zamani na meneja wa Ujerumani Jurgen Klinsmann ametimuliwa katika nafasi ya ukocha wa timu ya taifa ya Marekani.
Klinsmann mwenye miaka 52 aliyeshinda kombe la dunia akiwa mchezaji mwaka 1990 alianza kukinoa kikosi cha Marekani mwaka 2011.
''Tunaendelea kuwa imara, tuna wachezaji wa kiwango cha juu wa
kutusaidia kufuzu kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi,'' amesema Rais
wa shirikisho la soka nchini Marekani Sunil Gulati.
Klinsmann aliifikisha Marekani hatua ya 16 katika kombe la dunia 2014 nchini Brazil.
Sambamba na hilo walipoteza kwa magoli 2-1 wakiwa nyumbani dhidi ya
Mexico na baadae kufungwa 4-0 na Costa Rica katika hatua ya kufuzu kombe
la dunia.
Marekani inabakia mkiani mwa timu sita ikiwa haina alama yoyote.
Klinsmann mshambuliaji wa zamani wa Tottenham alihusishwa kuinoa timu ya
taifa ya England baada ya Sam Allardyce kubwaga manyanga mwezi
Septemba.
No comments:
Post a Comment