Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akikaribishwa na
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Idara ya Polisi ambaye pia ni Naibu
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (DIGP), Abdurahman Kaniki (aliyevaa tai)
kwa ajili ya kufungua kikao cha Baraza hilo, kinachofanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam. Picha na zote Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), Mwenyekiti wa
Baraza la Wafanyakazi Idara ya Polisi ambaye pia ni Naibu Mkuu wa Jeshi
la Polisi Nchini (DIGP), Abdurahman Kaniki (wapili kulia), Kamishna wa
Fedha wa Jeshi hilo, Albert Nyamhanga (kushoto) na Katibu wa Baraza
hilo, Merise Mwanyema wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima kabla ya Naibu
Waziri kufungua Kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Wajumbe wa
Baraza la Wafanyakazi Idara ya Polisi (hawapo pichani) wakati alipokuwa
anatoa hotuba ya ufunguzi wa kikao cha Baraza hilo kilichofanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika
hotuba yake, Masauni aliwataka wajumbe hao kufanya kazi kwa vitendo kwa
kuyatekeleza ipasavyo maazimio ya kikao hicho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la
Wafanyakazi Idara ya Polisi wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima kabla ya
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
kufungua Kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Baraza la
Wafanyakazi Idara ya Polisi ambaye pia Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi
Nchini (DIGP), Abdurahman Kaniki akizungumza na Wajumbe wa Baraza hilo
(hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia meza kuu) kufungua
Kikao cha Baraza hilo, kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Kamishna wa Fedha
wa Jeshi hilo, Albert Nyamhanga na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi
wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Jeshi la Polisi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi
Idara ya Polisi kutoka Zanzibar, Shemsa Said akichangia mada katika
kikao cha Baraza hilo kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akijibu maswali ya waandishi wa
habari mara baada ya kufungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi Idara ya
Polisi kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Ukonga
jijini Dar es Salaam. Masauni aliwaambia waandishi hao, Jeshi la Polisi
linaendelea kupambana na madawa ya kulevya pamoja na kulinda usalama wa
raia na mali zao nchini ikiwa ni sehemu ya majukumu yao. Pia aliwataka
wajumbe wa Baraza hilo kufanya kazi kwa vitendo kwa kuyatekeleza
ipasavyo maazimio yote ya kikao hicho. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment