Tuesday, 29 November 2016

Ukweli kuhusu wacheza soka wa nchi za Afrika

 Wacheza soka wengi barani Afrika wanataka kumfanana Samuel Eto'o (kushoto)
Utafiti mkubwa kuhusu masuala ya soka duniani unaonyesha kuwa maisha miongoni mwa baadhi ya wanasoka wa afrika, yana tofauti kubwa na maisha ya wale walio na bahati ya kusakata soka kwenye vilabu vikubwa duniani.
Chama cha wacheza soka wa kulipwa cha kimataifa (Fifpro) ambacho ni sawa na chama cha wafanyakazi, kimefanya utafiti wa dunia nzima kwa karibu wanasoka 14,000 kwenye nchi 54, ambao ni utafiti mkubwa zaidi kuwai kufanywa.
Zaidi ya wachezaji soka 3000 ambao walishiriki kwenye utafiti huu ni kutoka nchi 13 za barani Afrika zikwemo, Botswana, Cameroon, Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, Misri, Gabon, Ghana, Ivory Coast, Kenya, Namibia, Afrika Kusini, Tunisia na Zimbabwe.
Huku vijana wengi wa Afrika wakiwa na ndoto ya kusakata soka sawa na Didier Drogba au Samuel Eto'o, takwimu zilizokusanywa na Fifpro zinaonyesha ukweli kuhusu maisha ya wacheza soka barani Afrika
Dhuluma za kimwili
Baadhi ya masuala ya kushangaza yaliyotokana na utafiti huo ni kuwa dhuluma za kimwili dhidi ya wachezaji barani, ndizo mbaya zaidi duniani
Wacheza soka nchini Ghana wako kweye hatari ya kushambuliwa kimwili mara kumi zaidi, na maafisa wa nyadhifa za juu kuliko wachezaji wengine.
Nchini Afrika Kusini na Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, uwezekano wa wachezaji kushambuliwa ni mara tatu zaidi kuliko viwango vyote duniani.
Jamhuri ya Demokrasi ya Congo ina uwezekano wa juu wa wachezaji kushambuliwa na mashabiki, wakati wa siku ya mechi huku Kenya ikichukua nafasi ya pili.
Utafiti pia ulionyesha kuwa wachezaji walio katika nafasi ya kuamrishwa kufanya mazoezi peke yao wako barani Afrika.
Mishahara duni
Katika upande wa malipo, asilimia 100 ya wanasoka nchini Ghana walisema kuwa walilipwa chini ya dola 1000 kwa mwezi.
Wachezaji wenye malipo bora zaidi barani Afrika ambao wanalipwa zaidi ya dola 1000 kwa mwezi, ni kutoka nchini Morocco, licha ya wao kukumbwa na changamoto za kukosa kufahamu hatma yao.

 Licha ya mafanikio ya vilabu kama Zamalek (juu), Misri ina malipo duni kwa mujibu wa utafiti
Ligi ya Misri inaonekana kuwa bora zaidi barani Afrika, kufuatia vilabu vyake viwili kushinda kombe la klabu bingwa barani Afrika.
Klabu ya Al Ahly imeshinda vikombe vinane , Zamalek vitano na TP Mazembe ya DRC pia ina vikombe vitano.
Licha ya hilo ligi ya Misri huwa na malipo duni zaidi kati ya ligi 13 zilizofanyiwa utafiti barania Afrika
Zaidi ya asilimia 90 ya wachezaji walisema kuwa walilipwa chini ya dola 1000.
Nchini Gabon, ambayo ndiyo itakuwa mwaandalizi wa mechi za taifa bingwa barani Afrika mwezi Januari, asilimia 96 ya wachezaji walilalamikia kucheleweshwa kwa mishahara.
Mikataba
Afrika ina wachezaji wengi zaidi wasio na mikataba, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, asilimia 40 ya wachezaji wanasema kuwa hawana makaratasi ya mikataba.

 Wacheza soka wa Afrika mara nyingi hupigwa picha wakisaini mikataba ng'ambo, lakini wenzao barani Afrika hawana mikataba
Nchi tatu ambazo zina matatizo ya mikataba ni pamoja na Cameroon kwa asilimia 65, Gabon kwa asilimia 60 na Ivory Coast kwa asilimia 60.
Matumaini
Utafiti huo, hata hivyo unaonyesha kuwa kuna matumaini.

 Wacheza soka nchini Ivory Coast hupewa muda mrefu zaidi wa kupumzika
Upande wa likizo zilizolipwa, Ivory Coast na Namibia ni mfano mzuri, kwa kuwa nchi hizo huwapa wacheza soka likizo za zaidi ya siku 30 zilizolipwa kila mwaka.
Hii ni tofauti na Misri ambapo asilimia 93 ya wachezaji wanasema kuwa wao hupewa chini ya siku 10 za likizo inayolipwa kila mwaka.
Nchini Tunisia asilimia 99.5 ya wachezaji hupewa siku moja kila wiki ya kupumzika.
Uhakika wa kazi
Wachezaji wengi barani Afrika uhofia hatma ya maisha yao ya baadaye.
Wakati wachezaji waliulizwa ikiwa walihisi kuwa na wasiwasi kwa kazi zao, 11 kati ya nchi 13 zilikuwa za Afrika.
Licha ya utajiri wao, Morocco na Gabon zina asilimia kubwa.
La kushangaza ni kuwa wachezaji nchini Zimababwe, nchi ambayo shirikisho la Kandanda linakumbwa na matatizo ya kifedha, hadi kutimuliwa kutoka kwa kombe la dunia la mwaka 2018 baada ya kushindwa kumlipa kocha, wachezaji walihisi kuwa na uhakika wa kazi kuliko nchi zingine 13 za bara Afrika.
Kupanga matokeoUtafiti wa awali wa Fifpro, unaonyesha kuwa kukosa kuwalipa wachezaji mishahra huenda ikawa sababu ya kuwepo visa vya kupanga matokeo.
Malipo duni yamesababisha kuwepo majaribio mengi ya kupanga matokeo ikiwa ni asilimia 8.3 kutokana na utafiti
Licha ya asilimia 10.1 kusema walifahamu kuhusu visa vya kupanga matokeo kwenye ligi, asilimia hiyo ilikuwa ya juu kidogo kuliko ya nchi za ulaya ambayo ni 9.8.
Nchi tatu kati ya nchi tano zilizoripoti visa vingi zaidi vya kupanga matokeo ziko barani Ulaya.
Rekodi mbaya ya DRC
Nchi ambayo hakuna mchezaji angependa awe mchezaji wa kulipwa ni Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Asilimia 89 ya wachezaji nchini DRC hawana mikataba.

Idadi ya wachezaji ambao wameshambuliwa na wachezaji wengine ni mara tatu zaidi nchini DRC.
Mmoja kati ya wachezaji wanne aanasema kuwa ameshambuliwa wakati wa siku ya mechi.
Mmoja kati ya wachezaji watano anasema kuwa amedhulumiwa na wachezaji wenzake na mara nyingi amelazimishwa kusaini mikataba
Dalili nyingine ya mazingira mabaya ya kazi ni kuwa zaidi ya nusu ya wacheza soka nchini DRC, wanasema kuwa wana siku moja ya kupumzika kila wiki.

No comments:

Post a Comment