Mauzo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam ( DSE) yameendelea kushuka
kwa wiki ya tatu mfululizo baada ya wiki iliyopita kuporomoka kwa
asilimia 87.
Katika wiki hiyo iliyoishia Novemba 25, DSE imeeleza kuwa mauzo hayo yalishuka kutoka Sh4 bilioni hadi kufikia Sh500 milioni.
Kushuka huko kwa mauzo kulitokana na kuyumba kwa idadi ya hisa
zilizouzwa na kununuliwa sokoni hapo kwa asilimia 85 kutoka hisa 671,
618 hadi 101, 809 wiki iliyopita.
Ripoti ya wiki ya mwenendo wa soko hilo iliyotolewa leo Jumatatu
(Novemba 28, 2016) inaeleza kuwa kushuka huko kwa mauzo kunaweza
kuhusianishwa na ongezeko la mauzo ya hati fungani zilizouzwa sokoni
hapo wiki hiyo.
No comments:
Post a Comment