Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Homa ya Ini na Matumbo wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Dk John Lwegasha akizungumza na waandishi wa habari LEO
kuhusu kuanza kwa uchunguzi na tiba ya homa ya INI (Hepatitis B) katika
hospitali hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Dk Hedwiga Swani
na Dk Eva Owisso wa Muhimbili wakifuatilia mkutano huo.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Dk Hedwiga Swai akifafanua jambo kwenye mkutano huo LEO
“Hatua hiyo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya pili Ukanda wa Afrika Mashariki katika udhibiti na tiba ya ugonjwa huo”
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Disemba Mosi mwaka huu inatarajia kuanza kufanya uchunguzi wa Virusi vya Homa ya Ini (Hepatitis B) na kutoa tiba bure ya ugonjwa
huo kwa kutumia dawa ya Tenofovir na hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi
ya pili Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya Rwanda katika udhibiti na
kutoa tiba ya ugonjwa huo.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Daktari Bingwa wa
Magonjwa ya Ini na Matumbo, John Lwegasha amesema ni wakati muafaka wa
watu kujitokeza na kupima afya zao kwa ujumla na kwa wale waliothirika
na ugonjwa huo wajitokeze ili kufanyiwa uchunguzi zaidi na kupata nafasi
ya tiba kulingana na miongozo ya tiba inavyoelekeza.
“Utaratibu
mwingine wa uchangiaji wa gharama za matibabu katika maeneo mengine ya
uchunguzi na tiba ikiwa ni pamoja na uchangiaji wa gharama za kumuona
Daktari utabaki kama ulivyo,” amesema Dk. Lwegasha.
Tatizo
la ugonjwa huo Tanzania, kwa mujibu wa Dk . Lwegasha inakadiriwa kuwa
watu wanane kati ya watu mia moja wana maambukizi ya ugonjwa huo na
kwamba kiwango hicho ni kikubwa zaidi ya kile kinachokadiriwa kwenye
maambukizi ya Ukimwi kitaifa ambacho ni asilimia pungufu ya sita.
“Katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili asilimia 60 ya wagonjwa wanaokutwa na
Saratani ya Ini mara nyingi imetokana na maambukizi ya virusi hivyo,”
amesema Dk. Lwegasha.
Kuhusu
tiba amesema kama ilivyo kwa ugonjwa wa Ukimwi , ugonjwa huo sugu wa
Homa ya Ini hauna tiba ya kuponya isipokua dawa zilizopatikana hadi sasa
zinaweza kupunguza kasi ya maambukizi mwilini na kuzuia madhara kwenye
Ini.
Ugonjwa
wa Homa ya Ini ( Hepatitis) unasababishwa na Virusi viitwavyo Hepatitis
B na maambukizi yaugonjwa huo yanashahabiana na njia ya maambukizi ya
ugonjwa wa Ukimwi kama vile kufanya ngono zisizo salama , kuchangia
sindano au vikatio, kupewa damu isiyopimwa , kupitia uzazi wa mama na
mtoto hasa wakati wa kujifungua.
No comments:
Post a Comment