Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi Juju Danda amesema chama hicho
kinakusudia kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali ya nchi
ili kujiimarisha na kupata wanachama wapya.
Danda ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi) wakati akizungumza na wanahabari juu ya hali ya kisiasa nchini.
Amesema kifungu namba 11 cha Sheria ya Vyama vya Siasa kinavipa haki
vyama vyenye usajili wa muda na wa kudumu kufanya mikutano ya hadhara
na maandamano kwa ajili ya kujitangaza na kutafuta wanachama wapya.
"Hizi ni salama tu kwa watawala.Muda ukifika tutangaza lini tunaanza, wapi tutaanzia na kuishia ili kukiimarisha chama.
"Mikutano ya ndani ya tumeshaifanya sana, sasa ni wakati wa mikutano ya
hadhara ili kuubarisha umma kinachoendelea," anasema Danda.
Hata hivyo mpango huo wa chama hicho hautofanikiwa kutokana na polisi
kwa nyakati tofauti kutangaza kupiga marufuku mikutano ya hadhara na
maandamano.
No comments:
Post a Comment