Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na
Uwekezaji,Profesa Adolf Mkenda (kushoto) akibadilishana mawazo na
Meneja Mradi wa BEST-DIALOGUE, Bw.Hans Determeyer (katikati) wakati wa
majadiliano yaliyohusu kuongeza kasi ya ubunifu na ukuaji wa
wajasiriamali kupitia sera wezeshi zenye kutekelezeka na (kulia) ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF),Bw. Godfrey
Simbeye. Picha na Mpiga picha wetu,Dar es Salaam.
Wadau wa masuala ya biashara wa
ndani na nje ya nchi wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa majadiliano
iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Uwekezaji ,Profesa
Adolf Mkenda (hayupo pichani), wakati wa majadiliano yaliyohusu
kuongeza kasi ya ubunifu na ukuaji wa wajasiriamali kupitia sera
wezeshi zenye kutekelezeka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Sekta Binafsi (TPSF),Bw. Godfrey Simbeye (kulia) akitoa taarifa juu
ya maendeleo ya sekta binafsi nchini, wakati wa majadiliano yaliyohusu
kuongeza kasi ya ubunifu na ukuaji wa wajasiriamali kupitia sera
wezeshi zenye kutekelezeka, wa pili kulia Meneja Mradi wa
BEST-DIALOGUE, Bw.Hans Determeyer , katikati ni Mkurugenzi wa Program ya
Kimataifa ya SEPT,Profesa Utz Donberger, (wa pili kushoto) ni Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda na Uwekezaji ,Profesa Adolf Mkenda na kushoto ni
Mkuu wa Kitivo cha Biashara Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS) ,Dk.
Ulingeta Mbamba.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na
Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda (kulia) akifungua majadiliano
yaliyohusu kuongeza kasi ya ubunifu na ukuaji wa wajasiriamali kupitia
sera wezeshi zenye kutekelezeka, (wa pili kulia) Meneja Mradi wa
BEST-DIALOGUE, Bw.Hans Determeyer , (katikati) ni Mkurugenzi wa Program
ya Kimataifa ya SEPT, Profesa Utz Donberger, (wa pili kushoto) ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF),Bw. Godfrey
Simbeye na (kushoto) ni Mkuu wa Kitivo cha Biashara Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDBS),Dk. Ulingeta Mbamba.
Na MAELEZO
Serikali imeshauriwa kuweka
mazingira ambayo yatasaidia kuwa na sera bora na mifumo mizuri ya
kisheria inayochangia kukuza sekta ya Ujasiriamali (SME) ambayo pia
itaongeza ajira, vipato vya wajasiriamali na taifa ili kupunguza
umasikini katika jamii.
Akizungumza hayo jijini Dar es
salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF),Bw.
Godfrey Simbeye amesema kuwa serikali inahitajika kuweka mazingira
yatakayo changia kuwa na sera ambayo inayolenga kukuza kwa haraka sekta
ya wajasirimali ili kukuza ajira, vipato vya wajasiriamali na pato la
taifa na kupunguza umasikini katika jamii.
“Sera iliyopo ya mwaka 2003 ya
kuendeleza ujasiriamali inahitaji kuboreshwa zaidi ili kwenda na wakati
ili kukuza na kuimarisha maendeleo ya sekta hii” alisema Bw. Simbeye.
Aidha Bw. Simbeye alisema kwamba
majadiliano hayo yaliwaleta wadau wa masuala ya biashara wa ndani na nje
ya nchi kama Kenya,Ghana, Uganda, Ujerumani, Uingereza,Ethiopia,
Rwanda, Uholanzi, Taasisi za Biashara, wasomi na wajasirimali na
wawakilishi kutoka UN kujadili namna ya kuwa na sera hiyo wezeshi.
Bw. Simbeye aliongeza kuwa
Tanzania imejikiwekea mikakati ya kuelekea katika uchumi wa viwanda,
hivyo serikali itambue kukuza vipaji vya wabunifu katika sekta ya
uzalishaji na ujasiriamali wadogo na wa kati kwa kupewa motisha ili
waweze kuhamasika kuibua mawazo mapya.
Kwa upande wake Katibu Mkuu
Wizara ya Viwanda na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda alisema kuwa sekta ya
ujasirimali ina mchango mkubwa kwa taifa, na serikali imekuwa karibu
katika kuhakikisha inazidi kuimarika na kutoa mchango mkubwa.
“Pamoja na mchango huu wa sekta
hii pia tunatambua kuna changamoto mbalimbali ambazo kwa kushirikiana na
wadau wa biashara tunaweza kuifanya sekta hii kuimarika zaidi na kuwa
na mchango mkubwa kuliko ilivyo hivi sasa,” alisema Prof. Mkenda
Aidha Prof. Mkenda alisema
serikali imeweka mazingira ambayo yanasaidia kukuza sekta hiyo ikiwemo
taasisi zote zinazohusika na masuala ya biashara zinafanya kazi ipasavyo
kusaidia wajasiriamali wadogo na wakati kuzidi kukua.
Prof. Mkenda alisitiza kuwa
serikali itaendelea kushishirikisha sekta hiyo ili kuhakikisha inafanya
kazi kwa karibu kwani ndio injini ya uchumi wa nchi.
Naye Meneja Mradi wa BEST
DIALOGUE,Bw. Hans Determeyer alisema maendeleo katika nchi yanakuja kwa
sekta binafsi kuwa na nguvupamoja na kuweka mazingira wezeshi kati ya
serikali na wafanyabiashara wenyewe.
“Majadiliano haya ni chachu kwa
mataifa mbalimbali yaliyoshiriki katika kuweka mikakati inayowezesha
kufikia malengo ya kiuchumi,” na kwa kufanya hivyo ni kusaidia kupunguza
hali duni za vipato kwa wananchi na nchi kwa ujumla” alisema Bw.
Determeyer.
Kwa upande wake Mhadhiri wa Chuo
Kikuu cha Wakatoliki nchini Ghana,George Kafui Agbozo alisema nchi za
Afrika ili ziweze kupiga hatua kiuchumi zinahitaji kuweka mazingira ya
kukuza wajasiriamali wadogo na wakati.
“Changamoto za ukuzaji
ujasirimali kwa nchi hizi za Afrika zinafanana hivyo ukikuza
ujasiriamali kuna nafasi kubwa na kupunguza umasikini,”alisema Bw.
Agbozo.
Majadiliano hayo yaliandaliwa na
TPSF, Kituo cha Utafiti wa Sera na Utetezi (CPRA),Chuo Kikuu cha Dar es
Salam Kitivo cha Biashara (UDBS),kwa kushirikiana na Mtandao wa Maarifa
na Ubunifu Afrika (iN4iN) kwa ajili ya kupata njia bora za kuendesha
ujasiriamali nchini.
No comments:
Post a Comment