Bw Trump amesema wawili hao hawataweza kuhama katikati ya mwaka wa shule.
Alikuwa akiongea na wanahabari waliokusanyika katika kilabu chake cha gofu cha Bedminster, New Jersey Jumapili ambapo alikuwa anakutana na maafisa wanaotarajiwa kujiunga na utawala wake.
Alisema yeye ataishi White House lakini mkewe Melania Trump na Barron mwenye umri wa miaka 10 atahama "punde atakapomaliza masomo."
Trump kwa sasa huishi na mkewe na mwanawe huyo wa kiumbe katika chumba kilicho juu kwenye jumba la ghorofa la Trump Tower jijini New York.
Barron husomea shule ya kibinafsi iliyopo jiji la New York.
Trump si rais wa kwanza wa Marekani hivi karibuni kuhamia White House akiwa na watoto wa umri wa kwenda shule.
Rais Barack Obama alipoingia madarakani, mabinti wake Malia na Sasha walikuwa na umri wa miaka 10 na 7.
Rais Bill Clinton alipohamia ikulu Washington, Chelsea Clinton alikuwa na miaka 12.
Watoto hao wote walihamia White House masomo ya kiendelea na walihudhuria masomo shule ya Sidwell Friends, shule ya kibinafsi iliyo kaskazini magharibi mwa Washington.
Trump ameendelea kukaa Trump Tower tangu ashinde urais, jambo ambalo limesababisha maafisa wa usalama kuimarisha ulinzi kwenye jumba hilo.
Kuna maafisa wengi wa usalama wanaozingira jumba hilo wakiwa na mbwa wa kunusa, na kuna pia vizuizi vya kiusalama.
Habari kwamba Melania na Barron hawatajiunga na Trump ikulu ya White House Januari zimewashangazaa baadhi ya Wamarekani lakini pia amesifiwa na baadhi wanaosema ni vyema kuweka mbele maslahi ya mtoto na malezi yake.
Msemaji wa shughuli ya mpito Jason Miller amesisitiza kwamba Trump na familia yake wako tayari kutumikia Wamarekani na kwamba ni sababu ya mtoto pekee inayomfanya kutohamia mara moja ikulu ya White House.
"Familia ya Kwanza huishi White House kama ishara muhimu kwa taifa letu na kwa ulimwengu wote," aliandika Pamela Benbow, mmoja wa watu kwenye Twitter. "Uamuzi wa Melania Trump unashangaza."
Wengi wamelitolea mzaha suala hilo wakisema ladha ya Bi Trump kuhusu mapambo ya nyumba ndiyo imemfanya kutotaka kuingia White House haraka.
Kunao pia wanaodai hiyo ni ishara huenda mambo si mazuri katika ndoa yake na Bw Trump.
Wake wa Rais wa Marekani ambao hawakukaa White House wakati wa uongozi wa waume zao ni wawili pekee; Martha Washington, kwa sababu ikulu hiyo haikuwa imejengwa, na Anna Harrison, kwa sababu mumewe alifariki kabla ya kuhamia ikulu.
Wapo wanaomuunga mkono Bi Trump.
"Vyema sana, hili ndilo jambo watoto wawajibikaji wanafaa kufanya kwa ajili ya mtoto wa umri wa Barron," mtu mwingine kwenye Twitter aliandika.
Si jambo la ajabu kwa Bi Trump kusisitiza umuhimu wa kumlea Barron. Wakati wa kampeni, mara kwa mara alikaa nyumbani kumtunza.
William Seale, mwanahistoria katika Chama cha Historia ya White House ambaye pia ni mwandishi wa kitabu cha The President's House (Nyumba ya Rais), anasema mke wa Rais Grover Cleveland, Frances Folsom Cleveland, aliishi tu White House msimu wa sherehe na hafla nyingi rasmi.
Rais huyo alinunua nyumba muhula wake wa kwanza ambapo Bi Cleveland alikaa mara nyingi.
Alizoea kuita nyumba yake "Oak View" ingawa ilijulikana sana kama "Red Top" kwa sababu ya paa jekundu.
Lakini mke huyo, aliyekuwa na miaka 21 alipoolewa na rais huyo wa miaka 49, alikuwa mwanamke wa kwanza kuolewa akiwa anaishi White House.
Bw Seale anasema suala la watoto kusubiri hadi wamalize mwako wa masomo shuleni lilikuwa la kawaida na halijamshangaza.
Alisema watoto wa Rais John Tyler, aliyemrithi William Henry Harrison baada ya kifo chake, hawakuhamia ikulu mara moja.
Mke wa James Madison, Dolley Madison, pia alimwachilia mwanawe kutoka kwa ndoa yake ya awali, Payne Todd, aendelee na masomo.
Kumekuwa na makundi mawili ya watoto wa umri wa kwenda shuleni White House miongo mitatu iliyopita: Chelsea Clinton, alikuwa na miaka 12 wakati huo, na Malia na Sasha Obama, waliokuwa na miaka 10 na saba mtawalia.
Walisafiri na wazazi wao baba zao walipoingia madarakani - lakini wote waliishi ikulu ya White House, katika barabara ya 1600 Pennsylvania Avenue tangu siku ya kuapishwa kwa baba zao.
Familia ya Obama ilipunguza tatizo hilo kwa kuwafanya mabinti wake wabadilishe shule mapema kwa kuhamia Washington mapema, wakati wa mapumziko mafupi, na wakaanza shule wiki chache kabla ya baba yao kuapishwa Januari 2009.
Bi Trump amedokeza wkamba ataangazia sana kumlea mwanawe Barron. Hili linadokeza kwamba hatafanya shughuli nyingi hadharani na za umma kama Bi Obama.
Kirasmi, majukumu ya mke wa rais huwa ni ya staha tu - anafaa kuwa mwenyeji White House, akiandaa na kuudhuria sherehe rasmi akiandamana au bila kuandamana na mumewe.
Karibuni, wake wa marais wamekuwa wakitafuta jambo la kufaa jamii la kujihusisha nalo. Bi Obama alikuwa anawatetea wasichana, na aliongoza kampeni ya Let Girls Learn, (Waache Watoto Wasome).
Lou Henry Hoover, mke wa Rais Herbert Hoover, alikuwa rais wa kwanza kujihusisha sana na masuala ya umma, anasema Bw Seale.
Mtangulizi wake, Eleanor Roosevelt, pia alishiriki sana masuala ya umma wakati wa utawala wa mumewe.
Lakini mke wa rais wa karibuni ambaye alionekana sana kutopenda majukumu ya hadharani ni Nancy Reagan, mke wa Ras Ronald Reagan.
Hata hivyo baadaye alishiriki sana na kuonekana kuwa na uwezo mkubwa kwa mumewe uongozini. Baadaye alifahamika sana kwa kampeni yake ya kukabiliana na dawa za kulevya licha ya kwanza alianza sana kama mke wa nyumbani.
Hilo limewahi kufanyika awali. Lakini si wakati mke wa rais bado yuko hai.
Bintiye Rais Thomas Jefferson, Martha Jefferson Randolph alichukua majukumu 1801, nayeAngelica van Burenakachukua majukumu ya mke wa rais baada ya kuolewa na mwana wa kiume wa Rais Martin van Buren mwaka 1838. Marais hao wawili walikuwa wamefiwa na wake zao karibu miaka 20 awali.
Hata hivyo, je Ivanka Trump, ambaye alielezwa kuwa kama "mke mwingine" wa babake na jarida la Vanity Fair wakati wa kampeni - anaweza akachukua baadhi ya majukumu kutoka kwa mamake wa kambo?
Ivanka ni binti wa mke wa kwanza wa Bw Trump, Ivana.
Kuna mfano miaka ya karibuni. Chelsea alitekeleza baadhi ya majukumu ya mamake miaka ya mwisho ya utawala wa babake, Bi Clinton alipoangazia zaidi siasa.
Mazingira ya White House yanategemea familia
Chelsea wakati mwingine alikuwa anafanyia kazi ya ziada ya darasani katika afisi ya rais Oval Office. Hata aliwakaribisha marafiki zake walale ikulu.
Hillary Clinton na Michelle Obama walitekeleza majukumu yao kuwafaa watoto wao.
Familia zote mbili ziliwahimiza wanahabari kuheshimu usiri wa mabinti hao, na hilo liliheshimiwa.
No comments:
Post a Comment