Shirikisho la soka barani Africa (Caf) limetoa orodha ya majina ya
wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2016, jina la
mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta halipo katika
orodha ya wachezaji hao waliofanikiwa kuingia tano bora.
Samatta alikuwepo kwenye orodha ya awali safari hii alikuwa akiwania
tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa ujumla baada ya msimu uliopita kushinda
tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wa ndani wakati akiitumikia
klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Nahodha huyo wa Stars anaecheza klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji amewaacha
wachezaji wanaocheza kwenye vilabu vya Bundesliga, Premier League, na
Serie A.
Orodha ya wachezaji watano wanaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika
Pierre-Emerick Aubameyang of Gabon and Borrusia Dortmund
Riyad Mahrez of Algeria and Leicester
Sadio Mane of Senegal and Liverpool
Mohamed Salah of Egypt and Roma
Islam Slimani of Algeria and Leicester
Wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani.
Khama Billiat of Mamelodi Sundowns and Zimbabwe
Keegan Dolly of Mamelodi Sundowns and South Africa
Rainford Kalaba of TP Mazembe and Zambia
Hlompho Kekana of Mamelodi Sundowns and South Africa
Denis Onyango of Mamelodi Sundowns and Uganda
No comments:
Post a Comment