Benki ya Twiga Bankcorp imeanza msako wa wadaiwa sugu wa benki hiyo
ambapo kiasi cha shilingi bilioni 8 hazijarejeshwa na wateja waliochukua
mkopo katika benki hiyo ambayo kwasasa ipo chini ya usimamizi wa benki
kuu ya Tanzania BOT. Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya benki hiyo
kuanza tena kutoa baadhi ya huduma kwa wateja wake.
Msako wa wadaiwa sugu wa benki Twiga Bankcorp umeanza rasmi jijini Dar
es salaam, ukiwa chini ya kampuni ya ufilisi ya MARCAS. Msako huu
umeanza katika maduka ya wadaiwa wa benki hiyo eneo la Segerea jijini
Dar es salaam.
Mkurugenzi wa kampuni ya Ufilisi ya MARCAS inayohusika na ukusanyaji wa
madeni ya Twiga Benkcorp Richard Paul ameelezea lengo la msako huo.
“Zoezi hili ni endelevu, zoezi hili litafanyika Tanzania nzima kwa wale
wote waliokopa ndani ya benki ya Twiga nakukimbia na hizo pesa za Twiga.
Zoezi hili ni endelevu na litaanza hapa,tukafunga maduka
Kariakoo,tukaenda mpaka kwenye nyumba za vigogo waliokopa hela benki na
watu wote waliokopa hela benki tumewakamata,”alisema Paul.
Oktoba 28 mwaka huu, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa
Benno Ndulu alitangaza benki hiyo kumilikiwa na kuchukua usimamizi na
benki kuu ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment