Rais mteule wa Marekani Donald Trump anaendeleza harakati za uteuzi wa
maafisa wakuu anaopanga kuwajumuisha katika serikali mpya baada ya
kuapishwa tarehe 20 Januari.
Trump ameandika ujumbe mtandaoni kupitia akaunti yake ya Twitter na
kupendekeza uteuzi wa jenerali mstaafu James Mattis kusimamia wizara ya
ulinzi.
Trump aliarifu kuchukua uamuzi huo baada kufanya mazungumzo na Mattis kwa kumuona kuwa afisa mkuu anayefaa kuongoza wizara hiyo.
Katika kipindi chake cha miaka 44 alichohudumu kama jenerali wa kikosi
cha jeshi, Mattis alichangia pakubwa uvamizi wa Marekani nchini
Afghanistan na Iraq.
Mattis ambaye pia alihusika na mashambulizi ya Felluji Iraq mwaka 2004,
aliwahi kukashifiwa baada kununuliwa akisema kwamba hufurahia akiua
watu.
No comments:
Post a Comment