Waendeshaji baiskeli, Pikipiki na magari katika mji mkuu wa Burundi
Bujumbura wataanza kulipa ada ya kuegesha. Serikali inanuia kukusanya
mapato zaidi baada ya wafadhili wa magharibi kukata msaada wake kwa nchi
hiyo.
Nchi za magharibi zinazofadhili Burundi zilighathabishwa na hatua ya
Rais Pierre Nkurunziza kuwania Urais kwa muhula wa tatu, pamoja na
kutumia nguvu kuzima maandamano.
Serikali pia imefuta ufadhili wake kwa Vyuo Vikuu na badala yake
wanafunzi wote watagharamia ada za masomo punde wakiajiriwa baada ya
kufuzu.Ada mpya za kuegesha katika jiji kuu ni dola mbili kwa baisikeli
na dola 60 kwa malori makubwa.
Mabasi ya uchukuzi wa umma yatalipa dola sita kwa mwezi. raia wengi
wanahofia ada mpya huenda zikasababisha mfumuko wa bei ya bidhaa.
Wakaazi wengi katika mji mkuu tayari wanalalamikia ongezeko la gharama
ya maisha na wafanyikazi wengi hupokea dola 80 kwa mwezi.
Muungano wa Ulaya ulisimamisha msaada kwa serikali ya Burundi na kusema
Mamlaka hazijasaidia kurejesha utulivu nchini.Msaada wa Muungano wa
ulaya kwa Burundi ulikadiriwa kuwa dola milioni 470 kati ya mwaka 2014
hadi mwaka 2020.
Zaidi ya watu 400 wameuawa na wengine laki mbili unusu kukimbilia katika
nchi jirani kufuatia machafuko ya kisiasa yaliyozuka baada ya Rais
Nkurunziza kuamua kuwania mhula wa tatu.
Mwezi uliopita Burundi ilitangaza kujiondoa kutoka uwanachama wa
mahakama ya kimataifa ya jinai ICC.Tangazo hili lilitolewa miezi sita
baada ya mwendesha mashtaka mkuu wa ICC kusema atachunguza ghasia nchini
humo.
No comments:
Post a Comment