Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara |
Maafisa wa uchaguzi nchini Ivory Coast wamesema kwamba upande uliounga
mkono kielelezo cha katiba umeshinda katika kura ya maamuzi ya hapo
Jumapili kwa asilimia 93.
Asili mia 42 ya wapiga kura walijitokeza kwenye zoezi hilo lililosusiwa
na makundi ya upinzani. Rais Alassane Ouattara ameongoza kampeini ya
kuunga mkono mageuzi ya katiba. Moja wapo ya kipengee kilichobadilishwa
ni ulazima wa wagombea wa Urais kuwa na wazazi asilia wa nchi hiyo.
Upande uliounga mkono umeshinda |
Wapinzani wanasema Rais Ouattara anatumia mageuzi ya katiba kumteuwa
mrithi wake. Kumekua na maandamano ya upinzani kupinga mageuzi ya
katiba.Katika eneo lenye ufuasi wa chama cha upinzani cha 'Ivorian
Popular Front', mjini Abidjan, vijana waliharibu vituo vya kupigia kura.
Rais Alassane Ouattara amesema katiba mpya itasaidia kuunganisha taifa
na kumaliza tisho la kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe. Katiba mpya
imeondoa umri wa mgombea Urais na kuweka mihula miwili pekee ya Rais.
Pia kutakua na Baraza la Senate ambalo litashirikiana na bunge katika
kutunga sheria. Kuna nafasi ya Makamu wa Rais na katiba mpya inatambua
Baraza la Machifu wa kijamii. Tangazo la matokeo ya kura ya maoni
limetolewa na Rais wa tume ya uchaguzi Youssouf Bakayoko.
No comments:
Post a Comment