Urusi imetangaza kwamba itashindwa kukamilisha maandalizi ya viwanja
viwili vya kombe la dunia la FIFA 2018 vilivyotarajiwa kuwa tayari
Desemba 2017.
Kulingana na maelezo yaliyotolewa, viwanja hivyo ambavyo ni Nizhniy
Novgorod na Volgograd vimebainishwa kwamba hatoweza kukamilika kwa muda
unaotakiwa ambao ni Desemba 2017.
Kamati ya maandalizi ya kombe la dunia imetoa maelezo na kuarifu
matumaini yao ya kukamilishwa kwa viwanja vingine vitakavyochezewa mechi
za mashindano hayo.
Urusi iliwahi kutangaza mpango wa kupunguza bajeti ya maandalizi ya
kombe la dunia la FIFA 2018 kwa kiwango cha fedha ruble bilioni 3.
Mashindano ya kombe la dunia la FIFA 2018 yanatarajiwa kung’oa nanga
tarehe 14 Juni 2018 nchini humo na mechi zote kuchezwa katika viwanja 11
vya soka.
No comments:
Post a Comment