Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba, amesema serikali inatambua
umuhimu wa askari polisi na ndio maana ina mkakati wa kuliwezesha jeshi
hilo vitendea kazi bora.
Waziri Nchemba ameyasema hayo Jumatano hii alipokuwa akitoa ufafanuzi wa
matukio ya kuvamiwa kwa askari kujeruhiwa au hata kuuawa.
“Serikali inatambua umuhimu wa askari polisi, wanapokuwa katika kutimiza
majukumu yao ya kila siku. Napenda kulihakikishia bunge lako tukufu
kwamba serikali itaendelea kuliwezesha jeshi la polisi hapa nchini kwa
vitendea kazi bora na kuwajengea uwezo askari wetu kwa mafunzo ili
waweze kukabiliana na matukio ya uhalifu yanayohusisha uvamizi wa askari
polisi,” alisema Nchemba.
“Kwa sehemu ya pili jeshi la polisi limefanikiwa kukamata silaha 19 kati
ya 23 zilizoporwa kutoka kwa askari waliovamiwa wakiwa katika majukumu
yao katika kipindi cha Julai 2015 hadi Septemba 2016,” aliongeza.
No comments:
Post a Comment