Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa FAT na klabu ya Simba, Mwina Kaduguda
amewaambia matajiri wa Simba na Yanga akiwemo Yusuph Manji na Mohammed
Dewji kuwa wasidhani kuwa pesa inaweza ikamaliza matatizo ya mpira
nchini.
Akiongea na kipindi cha Sports HQ ya EFM, Kaduguda amesema kuwa pesa
haiwezi kusaidia mpira wa Tanzania kwa kuwa kwenye shirikisho la TFF
kuna viongozi ambao hawana sifa za kukaa kwenye nafasi hizo.
“Napenda kuwaambia Manji na Dewji kuwa pesa haiwezi ikauokoa mpira wa
Tanzania, wao wanajua kuwa pesa inaweza ikamaliza kila kitu. Angalia
Abrahamovic pale Chelsea anaimiliki timu lakini kawaachia viongozi ambao
wanaiendesha,” amesema Kaduguda.
“Tukubali tukatae TFF kuna viongozi hawana sifa za kuwepo pale lakini
ukionekana kiongozi mzuri wanakupinga. Nina uhakika kama Manji angeweza
kuangalia zaidi kwenye uongozi kuliko kwenye pesa, leo hii timu hiyo
ingecheza nusu fainali au mpaka fainali ya kombe la Shirikisho Afrika.”
No comments:
Post a Comment