Wanafunzi wameanza kuondoka kutoka Chuo Kikuu cha Makerere baada ya Rais
Yoweri Museveni kutangaza kifungwe mara moja Jumanne jioni.
Rais alisema amechukua hatua hiyo "kuhakikisha usalama wa watu na mali."
Chuo kikuu hicho kilikuwa kimekumbwa na vurugu kutokana na mgomo wa wahadhiri na wanafunzi.
Chama cha wahadhiri Jumatatu kiliamua kuendelea na mgomo hadi wahadhiri
walipwe marupurupu ya miezi minane ambayo yamefikia Sh32bn (dola 9.2
milioni za Marekani).
Wanafunzi walijiunga na mgomo Jumanne, na walitaka kukutana na Rais
Museveni badala ya mwenyekiti wa baraza simamizi ya chuo chini ya
uenyekiti wa Dkt Charles Wana-Etym.
Naibu chansela wa chuo hicho Prof Ddumba Ssentamu wiki iliyopita alikuwa
amewasihi wahadhiri wakubali kurejea kazini huku suluhu ya kudumu
ikiendelea kutafutwa.
No comments:
Post a Comment