Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais – Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba akiangalia
baadhi ya sampuli za mifuko isiyoharibu mazingira ambayo inatengenezwa Na Umoja wa Watengeneza mifuko isiyoharibika Tanzania (UWAMITA) Kulia
ni Mwenyekiti wa kikundi hiko Jumanne Mgude.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais – Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba, akiongea na
Wanakikundi wa Umoja wa Watengeneza Mifuko isiyoharibika Tanzania
(UWAMITA) walipomtembelea Ofisini kwake mtaa wa Luthuli.
MICHEZO YA KUBAHATISHA (BETTING)
Na Chrispino Mpinge
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limepokea kwa mshtuko taarifa za kuwepo makundi Ya watu
na makampuni wanaochezesha michezo ya kubahatisha inayohusu mashindano
mbalimbali yanayoandaliwa na kusimamiwa na TFF (betting).
TFF inauthibitishia Umma wa
watanzania kuwa Shirikisho halihusiki wala halijawahi kutoa kibali
chochote cha kuhusisha mashindano yake na michezo ya kubahatisha.
Kwa kuwa baadhi ya wahusika wa matendo hayo ni makampuni ya nje ya nchi hivyo TFF imechukua hatua zifuatazo:
1.TFF imeandika barua kwenye
Shirika la Bahati Nasibu ya Taifa ili kupata mwongozo wa kisera na
kisheria kuhusu haki na majukumu ya Shirika hilo katika kudhibiti na
kusimamia jambo hilo.
2.TFF imeandika barua kwa kitengo
cha sheria cha FIFA ili kupata mwongozo na ushauri wa Namna ya
kudhibiti makampuni ya nje yanayoshiriki mchezo huu.
TFF inawaomba wadau wa mpira wa
miguu na washiriki wa michezo ya kubahatisha wajiepushe Kushiriki
michezo ya kubahatisha inayohushu michezo yote inayoandaliwa na TFF.
WWF KUSAIDIA UJENZI WA MAJIKO SANIFU KATIKA SHULE TATU ZA MANISPAA YA MOSHI NA KUWEKA SOLAR KATIKA ZAHANATI YA MSARANGA.
Shule
ya Sekondari , J.K Nyerere iliyopo manispaa ya Moshi ni moja kati ya
shule zitakazonufaika na msaada wa kujengewa majiko sanifu na Shirika la
kimataifa la Mazingira (WWF-Tanzania)
Mratibu
wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira
,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akiongozana na wa wakuu wa idara
katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi walipotembelea shule ya
sekondari J.K Nyerere .
Mratibu
wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira
,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako wakiwa katika jiko la shule hiyo
kuangalia namna ambavyo wanaweza kupunguza matumizi ya kuni kupikia.
Matumizi
ya kuni ni makubwa katika shule za msingi ambazo zimekuwa zikitumika
kupikia hali inayochangia ongezeko la uharibufu wa mazingira kwa kukata
miti.
Mratibu
wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira
,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akitia saini katika kitabu cha
wageni katika shule hiyo ,katikati ni mkuu wa shule hiyo , Parfectius
Mushi akimtizama na kulia ni afisa kutoka WWF ,
Mratibu
wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira
,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako (kulia) akiwa na kaimu mkuu wa
shule ya msingi Langoni ,Mwl Hamad,alipotembelea kujionea namna gani
wanavyoweza saidia katika ujenzi wa majiko sanifu.
Mratibu
wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira
,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akiwa ameongozana na wakuu wa idara
za Halmashauri ya manispaa ya Moshi kutembelea jiko lilopo katika shule
ya msingi Langoni mjini Moshi.
Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akimueleza jambo Meneja Mradi wa ICLEI Africa Irina Velasco walipotembelea jiko la shule hiyo.
Mratibu
wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira
,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akitia saini katika kitabu cha
wageni katika shule ya msingi Msandaka alipotembelea shule hiyo.
Mratibu
wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira
,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akiongozwa na kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Danford Kamenya wakielekea kutizama
jiko la shule hiyo.
Jiko la shule ya msingi Msandaka.
Mratibu
wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira
,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akiwa katika picha ya pamoja na
wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Msandaka katika
manispaa ya Moshi.
Baadhi ya wanafunzi katika shule hiyo wakiwa katika chombo maalumu cha kuhifadhia nafaka shuleni hapo.
Diwani
wa kata ya Ng’ambo ,Genesis Kiwhelu akisalimiana na Irina Velasco wa
ICLEI alipowapokea katika zahanati ya Msaranga ambapo ujumbe wa WWF
ulifika kuangalia namna ya kuisadia zahanati hiyo vifaa vya Nishati ya
Umeme unaotokana na jua.
Mratibu
wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira
,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akitembelea katika zahanati hiyo.
Mratibu
wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira
,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akisikiliza maelezo kutoka kwa
mganga kiongozi wa zahanati ya Msaranga Dkt Para.
Mratibu
wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira
,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako na ujumbe wake wakiwa katika eneo
la kata ya Ngangamfumuni ambako WWF imepanga kuotesha miti.
Afisa
Habari wa manispaa ya Moshi,Ramadhan Hamisi akieleza jambo kwa ujumbe
huo mara baada ya kutizama eneo litakalo oteshwa miti.
No comments:
Post a Comment