
Na Kalonga Kasati
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine
Mahiga amesema Tanzania na Vietnam zimeahidi kuendeleza ushirikiano
katika nyanja mbalimbali kufutia makubaliano
yaliyofanyika wakati wa ziara ya Rais wa Vietnam nchini.
yaliyofanyika wakati wa ziara ya Rais wa Vietnam nchini.
Waziri Mahiga ameyasema hayo leo
jijini Dar es Salaam alipokutana na waandishi wa habari Wakati wa Majumuisho ya ziara ya siku nne ya Rais wa Vietnam nchini Mheshimiwa
Truong Tan Sang.
Akiwa ameongozana na Waziri
Habari na Mawasiliano wa Vietnman Nguyen Bal Son ameyataja Maeneo
ambayo Tanzania na Vietnam zimekubaliana kushirikiana kuwa ni uwekezaji
wa kilimo cha mpunga, uvuvi wa samaki wa ziwani na baharini na
uanzishwaji wa viwanda vya kusindika mazao ya biashara.
“Tumekubaliana kushirikiana
katika maeneo kadhaa ikiwemo kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia,
kuongezeka kwa uwekezaji kutoka Vietnam kwani kwa sasa biashara
inayofanyika kati ya Vietnam na Tanzania ni dola milioni 300 kwa mwaka,
tumekubaliana ifikie dola bilioni 900 ifikapo mwaka 2020”
Aidha, maeneo mengine ya
ushirikiano ni pamoja na kufungua mahusiano ya mawasiliano na elimu,
ambapo kutakua na fursa kwa wanafunzi wa Kitanzania kwenda kusoma nchini
Vietnam, na Wataalamu wa Vietnam kuja kufanya kazi pamoja na watanzania
na kusema kuwa kampuni ya Simu ya Halotel imefungua mlango kwa Vietnam
kuwekeza nchini na kuongeza kuwa lengo la Ushirikiano huu ni kuwa na
uhusiano ulio sawa na kila mmoja anufaike na mahusiano hayo.
Hata hivyo, Mahiga amesema kuwa
pamoja na maeneo kadhaa waliyokubaliana jambo la msingi Ni
namna ambavyo nchi hizo zitatekeleza makubaliano hayo kwa kuwa na
mawasiliano ya karibu na kukutana mara kwa mara baina ya watendaji wa
Serikali hizo mbili.
Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang
Sang, aliwasili nchini machi 8 mwaka huu, ambapo alikutana Na Rais Mhe.
John Magufuli na kufanya mazungumzo Ikulu na kutia saini mkataba wa
kibiashara baina ya Tanzania na Vietnam.
Aidha, Rais Truong na ujumbe
katika ziara yake ya siku nne nchini alikutana na Mwenyekiti wa CCM
Jakaya Kikwete, alizungumza na jukwaa la wafanyabiashara na viongozi
wao, na pia alitembelea eneo la viwanda (EPZA) Ubungo jijini Dar es
salaam.
Vilevile, alifanya mazungumzo na
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai na
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein
ambapo walikubaliana kuwa na mahusiano ya karibu na visiwa vya Zanzibar
kwa ajili ya uwekezaji katika utalii na uvuvi wa samaki.
Kwa upande wake, Waziri wa Habari
na Mawasiliano wa Vietnam Mhe. Nguyen Bal Son amesema Nchi yake ina
historia nzuri ya ushirikiano na mahusiano ya kidiplomasia ya muda mrefu
yaliyo Asisiwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na hivyo
wataendeleza uhusiano huo na Tanzania pamoja na kushirikiana ili kukuza
uchumi wa nchi hizo.
No comments:
Post a Comment