Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi
Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Mkoa wa
Kilimanjaro kuwafikisha mahakamani madereva wote na makondakta
wanaowatoza abiria nauli kubwa tofauti na zilizopangwa na ofisi hiyo.
Hayo yamesemwa leo na Kaimu Afisa
Mfawidhi Bw.Tadei Mwita alipokuwa akijibu kero ya mkazi wa Mkoa huo kwa
njia ya simu iliyotolewa na Gazeti la Mwananchi Machi 04, mwaka Huu,iliyozungumzia Daladala zinazofanya safari zake kati ya Moshi Mjini
– Himo kuwatoza nauli ya Shillingi 1000 abiria Wnaoshuka Maeneo ya
Kiboriloni, Sango Pumuani na Kawawa road tofauti na Nauli iliyopangwa na
SUMATRA katika vituo hivyo.
“Kuanzia wiki ijayo wadau wote
Watakao kuja kuomba leseni kwa ajili ya usafirishaji wa abiria Ndani ya
mkoa huu watahitajika kuonyesha nauli watakazo toza abiria katika vituo
vya katikati kabla ya kufika kituo cha mwisho cha safari zao,”alisema
Bw.Mwita.
Bw.Mwita alisema hivi sasa
SUMATRA Mkoa wa Kilimanjaro imeanzisha utaratibu wa kuwataka wadau wote
wanaotarajia kuanza kutoa huduma za usafiri wa daladala mkoani hapo
kuonyesha nauli watakazo toza katika vituo vya katikati kabla ya kufika
kituo cha mwisho.
Hata hivyo Afisa huyo
aliwashauri wakazi wa maeneo kama kiboriloni kwa sasa kupanda Daladala
za Kiboriloni kwa kuwa zipo nyingi ili kuepuka usumbufu unaojitokeza.
Malalamiko yanayohusu upatikanaji wa haki kushughulikiwa kwa wakati
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi Farida
Khalfan (katikati) akizungumza na waandishi wa habari(Hawapo Pichani)
kuhusu utaratibu wa Wizara katika kupokea na kushughulikia malalamiko
yanayohusu upatikanaji wa haki kwa wananchi. Kushoto ni Mkurugenzi
Msaidizi sehemu ya malalamiko Grifin Mwakapeje na kulia ni Mkurugenzi
Msaidizi Ufatiliaji Haki Bi Mary Mrutu.
Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya
malalamiko kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Grifin Mwakapeje akitoa rai
kwa wananchi na wadau wa sekta ya Sheria kuendelea kutumia huduma
ambazo zinazotolewa na Wizara hiyo ili kuwezesha kupata haki kwa wakati.
Na Kalonga Kasati
Serikali imedhamiria kuendelea
kupokea na kushughulikia malalamiko ya wananchi Yanayowasilishwa ili
kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wakati.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini
Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Malalamiko kutoka
Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Griffin Mwakapeje Wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari.
Aidha , Mwakapeje amesema Wizara
hiyo imekuwa ikipokea malalamiko yanayohusu Ucheleweshwaji wa Utekelezaji wa amri mbali mbali zinazotolewa na Mahakama,Ucheleweshaji
wa Nakala za Hukumu na Mienendo ya mashauri baada ya kumalizika
mahakamani.
Malalamiko Mengine Yanahusu
msongamano wa Mahabusu, ucheleweshwaji wa Upelelezi,Wananchi kubambikiwa
kesi,Migogoro ya Ardhi navitendo vya rushwa.
Akizungumzia wajibu wa Wizara
hiyo Mwakapeje amesema ni kuyaratibu na kuyawasilisha kwenye taasisi
husika ili kupata muafaka wa malalamiko hayo kwa wakati.
Hatua nyingine inayochukuliwa na
Wizara katika kuwasaidia wananchi kupata haki kwa wakati, ni kutoa Msaada wa kisheria unapohitajika kwa mujibu wa sheria na taratibu
zilizopo ili kuwawezesha Wananchi kupata haki kwa wakati.
Katika kushughulikia malalamiko
hayo “Serikali inayo dhamira ya dhati yakuhakikisha kuwa Wananchi
wanapata Haki kwa wakati.” Amesema Mwakapeje.
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo Bi Farida Khalfan
akizungumzia Mfumo wa kupokea malalamiko amesema kuwa wananchi wanaweza
kufika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo mtaa wa Sokoine au kuandika
barua ili kuwasilisha malalamiko yao na yatafanyiwa kazi kwa wakati.
No comments:
Post a Comment