Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Na Katibu Mkuu
wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa
Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam. Maalim Seif
aliruhusiwa kutoka hospitalini jana na hali yake inaendelea vizuri.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Akizungumza na Katibu Mkuu
wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza Wa Rais wa
Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam. Maalim Seif
amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumjulia hali na kusema kuwa hali
yake ya kiafya inaimarika siku baada ya siku.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa
Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa
Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam mara baada ya
kumjulia hali jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amemtembelea na kumjulia Hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Mheshimiwa Maalim Seif Shariff Hamad, katika Hoteli ya Serena Jijini Dar
es salaam, ambako anapata mapumziko baada ya kuruhusiwa kutoka
hospitali ya Hindu Mandal alikokuwa amelzwa kwa matibabu.
Pamoja na kumpa mkono wa pole, Rais Magufuli amemuombea Maalim Seif Shariff Hamad kupona haraka ili aweze kuendelea na shughuli zake kama kawaida.
“Nilishtushwa sana na taarifa za kuugua kwako, lakini sasa nafurahi kukuona ukiwa mwenye afya Nzuri ikilinganishwa na taarifa nilizozipata hapo awali, nakupa pole sana” amesema Rais Magufuli wakati akimjulia hali hotelini hapo.
Kwa Upande wake Maalim Seif Shariff Hamad amemshukuru Rais Magufuli kwa ukarimu na Upendo aliouonesha kwa kumtembelea hotelini hapo, na amewahakikishia watanzania kuwa hali yake sasa inakwenda vizuri na inazidi kuimarika kila kukicha.
“Sasa hivi ninaweza kutembea vizuri, kufanya shughuli zote mwenyewe bila ya msaada wa mtu Yeyote yule, na ni matumaini yangu kwamba baada ya Muda Mfupi, hali yangu itarudi kama kawaida, nije nishirikiane na watanzania wenzangu katika kutekeleza majukumu ya nchi yetu” Maalim Seif alimweleza Rais Magufuli.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam
09 Machi, 2016.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam
09 Machi, 2016.
No comments:
Post a Comment