Na Tabu Mullah
Mshambuliaji
Mohamed Mkopi wa timu ya Tanzania Prisons amechaguliwa kuwa mchezaji
bora wa Februari kwa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu wa 2015/2015.
Mkopi
katika mwezi huo uliokuwa na raundi nne, alicheza mechi zote nne za
timu yake dhidi ya Mbeya City, Yanga, Mwadui na Mgambo Shooting. Alitoa
mchango mkubwa kwa timu yake katika mechi hizo ambapo zote ilitoka sare,
hivyo kupata jumla ya pointi nne.
Katika
mechi hizo ambapo Tanzania Prisons ilifunga mabao matatu, Mkopi
alifunga bao moja na kusaidia kupatikana mabao mengine mawili.
Mshambuliaji
huyo ambaye mpaka sasa amefunga mabao sita kwenye Ligi hiyo, aling’ara
zaidi katika mechi mbili kati ya hizo nne ambapo alichaguliwa kuwa
mchezaji bora.
Mkopi
ambaye ni mshambuliaji wa kati alichaguliwa mchezaji bora kwenye mechi
dhidi ya Mwadui iliyochezwa mkoani Shinyanga, na ile dhidi ya Yanga
iliyofanyika Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
Kwa
kunyakua tuzo ya mchezaji bora kwa Februari, Mkopi atazawadiwa kitita
cha sh. 1,000,000 (milioni moja) na wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya
Vodacom.
Wachezaji
bora wa miezi miwili iliyopita ni kiungo Thaban Kamusoko wa Yanga
(Desemba 2015), na beki Shomari Kapombe wa Azam FC (Januari 2016).
Mkutano Mkuu TFF Machi 12-13 Jijini Tanga
Mkutano Mkuu wa mwaka wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliokuwa ufanyike Mwezi
Disemba mwaka jana sasa utafanyika wikiendi hii Jumamosi na Jumapili tar
12-13 March 2016 jijini Tanga.
Ajenda za mkutano huu ni kwa
mujibu wa katiba ya TFF. Mkutano mkuu utahitimishwa kwa Uwekaji wa jiwe
la msingi la kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji vya uchezaji mpira,
kituo kitakachojengwa jijini Tanga.
Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa hoteli ya Regal Naivera.
Jokate awataka wasanii kusaidia Huduma ya afya ya Wazazi na Watoto
Mbunifu wa mavazi, msanii wa
filamu na mrembo maarufu nchini, Jokate Mwegelo akimbeba Mtoto
aliyezaliwa siku ya wanawake duniani katika hospitali ya Palestina
jijini. Jokate alitembelea wodi hiyo na kutoa msaada.
Mbunifu wa mavazi, msanii wa
filamu na mrembo maarufu nchini, Jokate Mwegelo akikabidhi Moja ya
msaada wake kwa mmoja wa mama aliyejifungua mtoto wakati wa maadhimisho
ya siku Ya wanawake duniani katika hospitali ya Palestina jijini.
Mmoja wa mofisa wa kampuni ya
Suining Zerong Commercial Trading, Shuxia B akizungumza kwa Niaba ya
kampuni hiyo. Kampuni hiyo inafanya kazi pamoja na kampuni ya Kidoti.
Jokate Mwegelo ambaye ni
mkurugenzi wa kampuni ya na mmoja wa maofisa wa kampuni ya Suining
Zerong Commercial Trading, Shuaijie Duan wakikabidhi cheti cha shukrani
kwa daktari mkuu wa hosptiali ya Palestina, Dk Kariamel Wandi.
Na Tabu Mullah
Mara Baada ya kutembelea wodi ya
wazazi ya hospitali ya Palestina na kutoa misaada mbalimbali kwa
wanawake waliojifungua wakati wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya
wanawake duniani, Jokate alisema kuwa sekta hiyo inakabiliwa na
changamoto nyingi na kutokana na Umuhimu wake, wadau wanatakiwa kusaidia
serikali.
Jokate alisema kuwa serikali
inafanya kitihada kubwa ya kuboresha sekta hiyo na kumpongeza Rais Dk
John Magufuli kwa kuelekeza nguvu na kufanikiwa kutatua tatizo sugu
lililokuwa linaisumbua la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili T-scan Matatizo kadhaa sugu katika.
“Kila Mmoja wetu anajua nini
maana ya afya, huwezi kufanya jambo lolote kama huna afya bora, Hivyo Matibabu bora ni muhimu, serikali inafanya vitu vingi katika kuondoa
kero za wananchi Wake ikiwemo suala la afya, nimeguswa na kuamua kuunga
mkono kupitia kampuni yangu ya Kidoti ambayo inazalisha viatu na nyewe,”
alisema Jokate.
Alisema kuwa amefuraishwa na
huduma ya wodi ya wazazi ya hospitali ya Palestina na ushirikiano Waliopata kuanzia Mganga mkuu wa manispaa ya Kinondoni na uongozi wa
hospitali hiyo kwa ujumla.
“Kama unavyojua, misaada mingu
uelekezwa kwenye hospitali kubwa kubwa tu, kuna hospitali na Zahanati
nyingi ambazo zinahitaji kusaidia, hivyo wasanii wenzagu, hii ni fursa
kwenu kurudisha Faida kwa jamii, si lazima utoe fedha, hata kuwaona
wagonjwa na kuwafariji,” alisema.
Alisema kuwa mikakati yake ni kuona anatembelea na kutoa alichonacho kwa hospitali na vituo vya afya mbalimbali nchini.
Mmoja wa maofisa wa kampuni ya
Kidoti, Shuxia Bi kutoka China alisema kuwa ni vizuri jamii Hasa Wasanii
wa muziki, filamu, warembo na wanamitindo kuunga mkono juhudi za
serikali katika kutatua matatizo kwa jamii yenye mahitaji maalum. Shuxia
alisema kuwa kupitia chapa ya Kidoti wanaamini watafikia wadau wengi
jijini nan je ya mkoa.
Dakitari Mkuu wa hospitali ya
Palestina, Kariamel Wandi aliimpongeza Jokate na kampuni yake kusaidia
wodi ya wazazi. “Tumefarijika sana, umeonyesha kuwa unajali, wengi
wameshindwa kufanya kama Unavyofanya pamoja na kuwa na nafasi hiyo,
naomba uwe na moyo huo huo,” alisema Wandi.
Wandi alisema kuwa Jokate
amewasaidia wakati muafaka kwani hadi anakamilisha kutoa Misaada Mbalimbali, Jumla ya watoto 26 walizaliwa katika hospitali hiyo. Kati
ya hao, 18 ni Wasichana na nane ni wavulana.
No comments:
Post a Comment