Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw.
Hussein Katanga (katikati) akisisitiza jambo wakati wa kikao cha
Mrejesho wa Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria kwa
wananchi Februari 1 hadi 3, 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja,
jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mtendaji Mkuu Mahakama Kuu, Solanus
Nyimbi na Kulia ni Msajili wa Mahakama ya Rufaa, John Lugalema Kahyoza
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw.
Hussein Katanga (katikati) akisisitiza jambo wakati wa kikao cha
Mrejesho wa Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria kwa
wananchi Februari 1 hadi 3, 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja,
jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mtendaji Mkuu Mahakama Kuu, Solanus
Nyimbi na Kulia ni Msajili wa Mahakama ya Rufaa, John Lugalema Kahyoza
Washiriki wa kikao cha Mrejesho
wa Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria kwa wananchi
Februari 1 hadi 3, 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja, wakifuatilia
kikao hicho leo jijini Dar es salaam.
Mmoja wa washiriki wa kikao hicho akichangia.
Na. Kalonga Kasati
Mahakama ya Tanzania imesema kuwa
inaendelea na mkakati wa kufanya maboresho ya miundombinu yake ili
kurahisisha utoaji wa huduma ya mahakama kwa wadau na wananchi kwa
wakati.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini
Dar es salaam na Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania Bw. Hussein Katanga
wakati wa kikao cha Mrejesho wa Wadau walioshiriki katika utoaji wa
Elimu ya Sheria kwa wananchi Februari 1 hadi 3 mwaka huu katika viwanja
vya Mnazi mmoja, jijini Dar es salaam.
Bw. Katanga amewaambia wadau hao
kuwa Mahakama ya Tanzania inaendelea kufanya mabadiliko ya huduma zake
kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka Serikalini pia kutoka
kwa wadau wa Haki wanaoiwezesha Mahakama kufanya maboresho hayo kwa
lengo la kukuza Utoaji wa Haki nchini.
Amesema ili kusogeza huduma
karibu na wananchi Mahakama itatekeleza Mpango mkakati wa miaka 5 wa
kuiwezesha kushirikiana kwa karibu zaidi na wadau na Taasisi za utoaji
Haki katika masuala yanayohusu shughuli za kila siku za utendaji wa
Mahakama nchini.
“ Mahakama tutaanzisha mpango wa
miaka 5 ambao utaanzisha mfumo wa wa kushirikiana na wadau wetu kwa
karibu katika mambo yanayohusu shughuli zetu ili kuwaondolea wananchi
usumbufu na upotevu wa muda pindi wanapofuatilia huduma” Amesema.
Amefafanua kuwa Mahakama
imeshaanza kujenga majengo mapya ya kisasa ya Mahakama za Mwanzo katika
maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mahakama ya mwanzo Kigamboni jijini na
Kawe zote za jijini Dar es salaam, Mahakama ya Wilaya ya Mkuranga na
Kibaha mkoani Pwani ili kurahisisha utoaji wa Haki.
“ Mahakama sasa tuko katika
mwelekeo mzuri wa kufanya mabadiliko, kwa kushirikiana na wataalam wetu
wa ndani wakiwemo Chuo Kikuu Ardhi , tunaendelea kujenga majengo mapya
ya Mahakama katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mahakama ya Mwanzo
Kigamboni, Mkuranga, Kibaha na Kawe ambayo yatakamilika ifikapo Juni
mwaka huu” Amesisitiza.
Bw. Katanga ameongeza kuwa mpango
uliopo ni kuhakikisha kuwa majengo yaliyopo yanakarabatiwa sanjali na
ujenzi wa majengo mapya katika Mahakama zote 133 nchi nzima.
Aidha, amebainisha kuwa Mahakama
inaendelea kujenga mazingira wezeshi kwa watumishi wake ikiwemo ununuzi
wa mabasi ya kusafirishia watumishi, magari madogo na Pikipiki ili
kuwawesha watumishi wa Mahakama kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa
Mahakama Kuu Solanus Nyimbi akizungumza na wadau hao amewataka wafanye
kazi kwa kushirikiana katika kuwahudumia wananchi ili kuongeza imani yao
kwa Mahakama.
Amezitaka Taasisi na wadau
wanaohusika na utoaji wa Haki kujikita katika kushughulikia matatizo ya
wananchi ili kufanikisha dhana ya Utoaji Haki kwa Wakati ili kwenda na
mpango uliowekwa na Mahakama wa kuondoa mrundikano wa mashauri
mahakamani na ule wa kuzifuta kesi zilizokaa muda mrefu.
Naye Msajili wa Mahakama ya
Rufaa, John Lugalema Kahyoza ametoa wito kwa Taasisi za Utoaji wa Haki
kukutana mara kwa mara ili kujdili na kutatua changamoto zinazoukabili
Utoaji wa Haki nchini.
No comments:
Post a Comment