Tuesday, 15 March 2016

Maboresho ya Uwanja wa Uhuru

1Muonekano wa nje wa Uwanja wa Uhuru.
2Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge akielekeza jambo kuhusu wavu Uliowekwa kwa ajili ya kuzuia mashabiki wasirukie na kuharibu miundombinu katika maeneo ya vyoo vya uwanja wa Uhuru jana wakati wa kikao cha ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.
3Msanifu wa Majengo na mbunifu wa Mchoro wa Uwanja wa Taifa Aloyce Peter Mushi akifafanua jambo wakati wa kikao cha ukaguzi wamaendeleo ya ujenzi wa uwanja huo jana jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Bibi. Cecilia Kasongo, Mhandisi wa Uwanja wa Taifa Yusuf,Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge, Muhandisi wa mradi wa ujenzi wa uwanja wa Uhuru E. Mwamakunga na Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio.
4Meneja wa Ujenzi wa Kampuni ya BCEG inayojenga uwanja wa Uhuru Zhang Jiawei akifafanua jambo wakati wa kikao cha ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo jana jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge,Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio, Msanifu wa Majengo na mbunifu wa Mchoro wa Uwanja wa Taifa Aloyce Peter Mushi Muhandisi wa mradi wa ujenzi wa uwanja wa Uhuru E. Mwamakunga.
5Wajumbe wa kikao cha kukagua na kutathmini maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Uhuru wakikagua miunndombinu ya majitaka inayoendelea kujengwa katika uwanja wa Uhuru jana jijini Dar es Salaam.
6Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio(mwenye suti nyeusi) akielezea jambo wakati wa kikao cha ukaguzi wa Maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa Uhuru jana jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment