Na Chrispino Mpinge
Siku
tatu baada ya kutoka India alikokwenda kwa ajili ya kupata matibabu,
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad jana
alilazwa katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassoro Mazrui amesema kuwa chanzo cha
Maalim Seif kulazwa katika hospitali hiyo jana asubuhi ni uchovu wa
safari yake ya India ambayo alienda kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa
mgongo.
Mazrui
alikanusha taarifa zilizokuwa zinaenezwa kwenye mitandao ya kijamii
kuwa kiongozi huyo wa CUF alilazwa kutokana na matatizo ya moyo. Alisema
kuwa hakuna kumbukumbu yoyote ya ripoti ya daktari inayoonesha kuwa
Maalim Seif ana tatizo la moyo.
Naibu
Katibu Mkuu huyo wa CUF alisema kuwa kiongozi huyo anaendelea vizuri
kiafya na kwamba hayuko katika hali mahututi kama ilivyokuwa ikielezwa.
“Anakula
na kufanya kila kitu mwenyewe na hata jioni hii nimeongea naye, anakula
kila kitu, hivyo Watanzania wasiwe na wasiwasi juu ya afya ya Maalim
Seif,” alisema Mazrui.
Viongozi
mbalimbali wa vyama vya siasa waliwasili katika hospitali hiyo kumjulia
hali akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim
Lipumba.
No comments:
Post a Comment