CHAMA cha mchezo wa mpira wa
wavu Mkoa wa Pwani (COREVA) kimeandaa kozi ya Mafunzo Ya walimu wa
mchezo huo yanayotarajiwa kufanyika kuanzia mwezi machi 24 hadi Aprili
1 mwaka huu wilayani Kibaha.
Akizungumza na Tanzania Daima
Katibu mkuu wa Chama hicho Lonjini Mzavas alisema kwamba Wameandaa kozi
hiyo kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa lengo la
kuweza kutoa mafunzo ambayo yataweza kusaidia kuwapata walimu wa
mchezo huo.
Aidha Katibu huyo alisema kwamba
kozi hiyo itawahusisha baadhi ya walimu wanaotoka katika shule za
msingi, sekondari pamoja na vyuo waliopo katika Mkoa wa Pwani ambao
kupitia kozi hiyo itaweza kuwajengea uwezo katika ufundishaji wa mpira
huo.
Alisema kwamba lengo lao kubwa
la kuandaa kozi hiyo ni kwa ajili ya kuwajengea uwezo walimu Wa
kuzitambua sheria na taratibu mbali mbai zinazotumika katika mchezo
huo wa wavu ili na wao waweze kuzitumia vema kwa kuweza kuwafundisha
wanafunzi mashuleni kwao.
“Ndugu mwandishi mchezo huu wa
mpira wa wavu katika Mkoa wetu wa Pwani ulikuwa upo nyuma sana lakini
kwa sasa tumejipanga na safu yangu ya uongozi kwa ajili ya kuhakikisha
tunajitaidi kutoa kozi mbali mbai amabzo zitaweza kuleta mabadiliko
chanya katika tasnia ya mchezo huu wa wavu,” alisema Mzava.
Katibu huyo alibainisha kwamba
katika kozi hiyo walimu hao watafundishwa mbinu mbai mbali kwa njia ya
vitendo pamoja na nadharia ili kuhakikisha kwamba pindi watakapomaliza
mafunzo Hayo watakuwa ni mabalozi wazuri katika kuutangaza mchezo wa
mpira wa wavu katika Mkoa wa Pwani na Taifa zima kwa ujumla.
Pia alisema kwamba walimu ambao
wanahitaji kushiriki katika kozi hiyo wanatakiwa kuchangia Gharama ya
kiasi cha shilingi 50,000 kwa ajili ya masuala mbali mbali ya vifaa,
chakula pamoja na mahitaji mengine ya msingi kwa ajili ya uendesheji wa
kozi hiyo.
Katika hatua nyingine alisema
kwamba kozi hiyo itafundishwa na mkufunzi kutoka chama cha Wavu Tanzania
(TAVA) na kuongeza Wilaya zote za Mkoa wa Pwani zitashiriki katika
mafunzo Hayo, ikiwemo, Bagamoyo, Kibaha, Kisarawe,Mkuranga,Rufiji,
pamoja na Mafia.
No comments:
Post a Comment