
Kamishna Jenerali wa Magereza
John C. Minja( wa pili kushoto) akikagua maeneo mbalimbali ya Gereza
Bukoba alipofanya ziara ya kikazi leo Machi 11, 2016 (wa kwanza kushoto)
ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera, SACP. Omari Mtiga (wa pili kulia)
ni Mkuu wa Gereza Bukoba, ACP. Benizeth Bisibe.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John
Mongella akiongea ofisini kwake na Kamishna Jenerali wa Magereza John C.
Minja na ujumbe wake (hawapo pichani)
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John
Mongella akiongea ofisini kwake na Kamishna Jenerali wa Magereza John C.
Minja na ujumbe wake kama inavyoonekana katika picha.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu
Kanda ya Bukoba Mhe. Sivangilwa Mwangesi Akisalimiana na Kamishna
Jenerali wa Magereza John C. Minja alipomtembelea ofisini kwake.
Kamishna Jenerali wa Magereza
John C. Minja (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa
Waandamizi wa Jeshi la Magereza Mkoani Kagera mara baada ya kutembelea
Gereza la Wilaya ya Bukoba (Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Na Mwandishi Wetu
Kamishina Jenerali wa Mageraza
nchini John Carmir Minja afanya ziara ya kikazi Mkoani Kagera yenye
lengo la kutembelea na kukagua Magereza ya Mkoa wa Kagera pamoja na
kujionea miradi ya uzalishaji inayosimamiwa na Jeshi hilo.
Akiwa Mkoani hapa Kamishna
Jenerali Minja alifika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John
Mongella na kufanya naye mazungumzo kuhusu utendaji kazi na ufanisi wa
Jeshi la Magereza Mkoani hapa katika kuimarisha ulinzi na usalama.
Aidha katika mazungumzo hayo
walizungumzia changamoto ya msongamano wa Mahabusu katika Gereza la
Wilaya ya Muleba ambalo hivi sasa linatumika kuhifadhi Mahabusu wa
Wilaya ya Muleba na Wilaya ya Chato Mkoani Geita ambayo haina Gereza la
Wilaya.
Kamishna Jenerali wa Mageraza
nchini John Carmir Minja pia alitembelea Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba na
kufanya mazungumzo na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo Mhe. Sivangilwa
Mwangesi juu ya namna ya kuongeza kasi ya usikilizwaji wa kesi
mbalimbali za watuhumiwa ili kuondoa msongamano Magerezani.
Vilevile Kamishna Jenerali Minja
alitembelea Gereza la Wilaya la Bukoba na kuongea na wafungwa na
Mahabusu wa Gereza hilo pia na kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la
zahanati ambalo lipo katika hatua za mwisho kukamilishwa ili liweze
kutoa huduma za afya kwa wafungwa na watumishi wa Jeshi hilo pamoja na
wananchi wanaoishi jirani na zahanati hiyo.
Kamishna Jenerali Minja yupo
Mkoani Kagera kwa siku 7 kuanzia tarehe 10 hadi 16 Machi, 2016 Ambapo
lengo la ziara hiyo ni kutembelea na kukagua Magereza ya Mkoa wa Kagera
pamoja na kujionea miradi ya uzalishaji inayosimamiwa na jeshi hilo.
No comments:
Post a Comment