Wamesema simba hao wanaodaiwa kuwa watatu na wazee ambao ina daiwa
wametoroka porini baada ya kushindwa kuwinda kutokana na uzee ambapo
wameshakula mbuzi zaidi ya ishirini kijijini hapo wamekuwa wakisumbua
katika kijiji hicho nyakati za usiku na kuwafanya waishi kwa hofu
wakihofia kuliwa na simba hao.
Mhifadhi wa wanyamapori katika wilaya ya tunduru Bw.Charles Shawa
anasema kuwa msako mkali wa kusaka simba unaendelea huku akisema ni
simba mmoja tu ndiye anayesumbua kijijini hapo.
Mkuu wa wilaya ya tunduru Bw.Chande Bakary Nalicho anasema nguvu
zimeongezwa katika msako wa simba ambapo kuna askari wanyamapori sita
katika msako wa simba.
No comments:
Post a Comment