Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
mkoani hapa kimesema uandikishaji wa majina ya wapiga kura kwenye
daftari la kudumu la wapigakura unaotakiwa kuanza leo mkoani hapa,
unafanywa kwa siri.
Mkurugenzi wa operesheni na mafunzo wa chama hicho ngazi ya taifa,
Benson Kigaila, alieleza hayo kupitia mkutano wa hadhara, uliyofanyika
kwenye uwanja wa barafu mjini hapa. Alisema Chadema kimeanza kufanya
uhamasishaji katika viunga vyote vya mji huo kwa kuingia nyumba hadi
nyumba na kuzungumza na mtu kwa mtu, kuhakikisha kila mwenye sifa ya
kupiga kura, anajiandikisha.
Alisema zoezi hilo litafanyika bila kujali tofauti za itikadi za
vyama vya kisiasa, kwa sababu Chadema inaamini lengo kuu ni kuikomboa
Tanzania kutoka katika manyanyaso yanayofanywa na viongozi wa CCM ambao
chama chao kimekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 50 huku nchi
ikiendelea kudidimia kwenye umasikini. Mkutano huo ulitangaza wanachama
wa Chadema wanaotarajia kuchuana katika uchaguzi wa ndani ili kupata
watakaokiwakilisha katika kugombea ubunge, kwenye majimbo yote tisa ya
mkoani Dodoma.
Jimbo la Chilonwa ambalo kwa sasa Mbunge wake ni Ezekiah
Chibulunje, ambaye ametangaza kung’atuka baada ya kulitumikia kwa miaka
20, ilielezwa mkutanoni hapo kuwa wana Chadema wanaoliwania ni pamoja na
Eva Mpagama, Manambaya Manyanya na John Kigongo.
Jimbo la Kongwa linalowakilishwa na Job Ndugai, ambaye pia ni Naibu
Spika wa Bunge la Tanzania, linawaniwa na Emmanuel Suday, Mashaka
Madale na Mussa Muhaha. Majimbo mengine ambayo yalielezwa kuwindwa na
chama hicho ni pamoja na Kibakwe, linalowakilishwa na Waziri wa Nishati
na Madini, George Simbachawene.
No comments:
Post a Comment