Zaidi
wa wananchi 6000 wa kata ya wazo jimbo la kawe na kata ya goba jimbo la
ubungo jijini dar es salaam hawana mawasilaiano ya barabara na huduma
ya UMEME baada ya mto Tegeta kufurika maji na kusomba daraja lao la muda
walilokuwa wanategemea kuvukia na kusababisha shughuli za kata hizo
kusimama.
Wakazi hao wamethirika zaidi kutokana na mto huo kufurika maji
huku ukiendelea kulika ukizifuata nyumba za wananchi na wakazi wa mtaa
wa muungano waliopo kata ya goba na mtaa wa kilimahewa waliopo kata
wazo,hali ambayo imewalazimisha kutumia kamba kwa ajili ya kuvuka huku nguzo ya umeme mkubwa
ikiwa inaninyinia katikati ya mto huo Jambo lilolazimu shirika la ugavi
wa umeme nchini kakata huduma ya umeme katika kata hizo.
No comments:
Post a Comment